Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka. (Alama 20)

 (8m 55s)
5314 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika ‘Tumbo lisiloshiba na Hadithi nyingine’, fafanua maudhui ya utabaka. (Alama 20)
Tumbo Lisiloshiba
a) Utabaka.
-Kuna tabaka la mabwanyenye na tabaka la wanyonge. Tabaka la
mabwanyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi, hii jitu kubwa linaonekana likisimamia shughuli ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporornoka.
b) Mapenzi ya Kifaurongo
Utabaka.
-Dennis anatoka katika familia maskini, Wazazi
wake walikua wachochole hawakua na mali yoyote. Walijitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana. .
-Dennis alikuwa mwanachuo wa tabaka la chini. Kulikuwa na wengine ambao walikua na fedha tele.
-Shakila alikuwa wa tabaka la juu. Mama yake alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la uchapishaji.
-Wanachuo waliotoka tabaka la juu walikua na maisha mazuri, libasi zao ni bora, wana simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine.
-Kulikuwa na watu walioendesha magari ya kifahari makubwa na mazuri.
-Wazazi wa Dennis ni wa tabaka la chini.
c) Ndoto Mashaka
Utabaka
-Kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao, bado hawajawahi kujinasua. Mwandishi anaonyesha kuwa katika mtaa wake, wamo rnaskini wengi. Na si humo tu, kuna sehemu nyingi nyinginezo.
-Chumba cha Mashaka kwa mfano, kimepakana na choo cha jirani. Maji ya kuogea
yanapita karibu na churnba chao.
-Tabaka la chini hubaguliwa. Mzee Rubeya anahamia na kurudi Yemeni maana hakuweza kustahimili aibu ya binti yake kuolewa na mchochole.
d) Kidege
Utabaka.
-Kuna tabaka la midege mikubwa. Hii ina nguvu na midomo yao ni kama mapanga.
-Midege mikubwa inavamia na kutwaa visamaki vilivyokuwa katika kidimbwi cha bustani ya llala.
Kuna tabaka la chini.
Tabaka hili la videnge vidogo linaungana na kupambana dhidi ya uvamizi wa midege. Hatimaye videge vinashinda na kuifukuza midege mikubwa.


|