Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya
b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza
c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.” Thibitisha.

 (8m 21s)
5025 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“… Ningeondoka shuleni mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya
-Haya ni maneno ya Jairo. Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu. Sherehe hii ilifanyika shuleni. Jairo anamkosoa mwalimu
Mosi kwa kumpatia matumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii.
b) Onyesha vile kinaya kinavyojitokeza
Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa matumaini maishani badala ya
kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo anadokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana ni lazima aibe au aue.
c) “ Kinaya kimetumika kwingine kwingi katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu.” Thibitisha.
-Ni kinaya kwa Jairo kudai ili mtu awe wa maana, athaminiwe na kuitwa
mheshimiwa na kuwa bingwa lazima aibe,apore au aue.
-Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
-Ni kinaya pia kwa Mwalimu Mosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosoa badala ya kumsifu.
-Ni kinaya kwa Jairo kuona elimu haina manufaa yeyote
ilhali wenzake walifaidi kutoka kwa elimu ya mwalimu wao.
-Ni kinaya kuwa baadhi ya wanaofunzwa shuleni na walimu waadilifu wanaendeleza ufisadi na uporaji. Jairo anasema wenzake kama Baraka, Festo, Mshamba na Nangeto ni wakora na utajiri wao ni zao la ukora
-Ni kinaya kwa jairo kumtoa bintiye na mkewe kama
zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa.
-Ni kinaya kwa jairo kudai kuwa pombe ni kiliwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masaibu ya maisha na kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
-Ni kinaya kwa mkewe Jairo kukukubali kitendo cha
mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine.
-Ni kinaya kwa jairo kudai kuwa ufuska ndio raha ya maisha na kuwa uadilifu haufai.


|