Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo Maudhui ya elimu.
b) Shagake dada ana ndevu .
c) Mame Bakari .

 (8m 41s)
11157 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jadili maudhui ya elimu katika Diwani ya Tumbo lisiloshima ukizingatia hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya kifaurongo
Maudhui ya elimu.
Elimu ya sekondari inaonyesha utabaka.Wanafunzi wa shule za kitaifa na mikoa ni wa tabaka la juu. Wazazi wao wana uwezo wa kugharamia masomo yao. Wale wa shule za vijijini ni wa tabaka la
chini. Wana matatizo ya karo kwa sababu ya umaskini.
- Utabaka pia unadhihirika katika elimu ya chuo kikuu cha kivukoni, wanafunzi wenye fedha wanadharau wenzao maskini.
- Elimu ya chuo kikuu inatatiza kwa kutowajibika kwa wahadhiri katika kazi yao. DKt Mabonga anakataa kuwajibu wanafunzi wake na kuwatamausha kiasi cha kutamani kukamilisha elimu
haraka wakashughulikie mambo mengine.
- Mapenzi huathiri matokeo ya mitihani ya mwanafunzi katika chuo kikuu. Dennis alifuzu vyema kwani mwanzoni hakuwa na mpenzi na hivyo alizingatia masomo.
- Elimu ndio njia ya pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis anatafuta kazi baada ya kukamilisha masomo.
- Elimu ndio njia ya pekee ya kumpatia mtu ajira. Dennis
anatafuta kazi baada ya kukamilisha maneno.
- Elimu ina jukumu la kutengeneza mustakabali wa maisha. Dennis anataka kusoma ndio awe profesa au daktari.
b) Shagake dada ana ndevu .
-Swala la elimu limeshughulikiwa na mwandishi wa hadithi hii.
-Mwandishi anadhihirisha kwamba bila kutia bidii
masomoni wanafunzi hawawezi kufaulu masomoni.
-Umuhimu wa majadiliano miongoni mwa wanafunzi katika maandalizi ya mtihani.
-Safia na kimwana wanasoma pamoja.
-Hadithi inalenga umuhimu wa wazazi kufuatilia jinsi ambavyo watoto wanavyosoma.
c) Mamake Bakari .
Katika hadithi hii elimu inaonekana kukubwa na changamoto mbalimbali.
i) Watoto wa kike kubaguliwa na walimu pamoja na wanafunzi baada ya kuwa wajawazito. Sara anaogopa kufukuzwa shuleni na mkuu wa shule.
ii) Kuwadharau na kuwadunisha wasichana wanaobeba mimba wakiwa shuleni.
iii) Badala ya walimu kuwapa ushauri nasaha wanawapiga vijembe na kuwadhihaki.
iv) Umuhimu wa bidii katika masomo sara na rafiki yake Sarina wanasoma masomo ya ziada
v) Twisheni inayofanyika usiku inahatarisha usalama wa wanafunzi .hili ndilo lililosababisha kubakwa kwa Sara.


|