Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.

 (4m 41s)
5821 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ukengeushi huzorotesha maendeleo ya kijamii. Jadili kauli hii ukirejelea hadithi ya ‘Mkubwa’.
Ukengeushi ni hali ya kuacha njia nyofu na kufuata njia potovu.
-Viongozi wa kisiasa wamekengeuka kuwa kuwaua vijana ambao ni nguvi ya taifa.
-Vijana wamepotoka Kimaadili- Mkubwa aliona vijana wanalaliana nje
hdharani, walipotambua wameonekana walikuwa tayari kuua watu kwa kisu au bisibisi.
-Vijana wamegeuka kuwa wezi na wanyanganyi watu mali zao.
-Vingozi wa serikali wanafanya biashara ya ‘unga’bila kujali athari kwa vijana na taifa.
-Viongozi wanajitajirisha kuwa kuuza unga, wanaingiza bidhaa hii bandarini bila kukaguliwa.
-Unga unasababisha vijana wengi kuwa wanyonge na wasio na akili timamu. K.m mkubwa anamkuta kijana aliyetoa denda mdomoni.
-Vijana ni wapyoro – wanatumia lugha chafu ajabu.
-Tamaa ya utajiri inamfanya mkubwa kuingilia biashara ya kuuza dawa za kulevya.
-Mkubwa anauza shamba lake la urithi na kupata milioni kumi ambazo anatumia kuhonga wapiga kura.
-Mkubwa anatoa rushwa kuwa kiongozi wa askari
waliokamata mzigo wake na pia mkumbukwa aachiliwe.


|