Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“..Wanafunzi wa chuo kikuu si kama watoto vikembe wa shule ya chekechea…..”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hili
c) Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua

 (7m 18s)
10613 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“..Wanafunzi wa chuo kikuu si kama watoto vikembe wa shule ya chekechea…..”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
Msemaji ni Dkt Mabonga
Msemewa - Wanafunzi wa somo la fasihi
Mahali – Ukumbi wa mhadhara
Sababu – Dkt Mabonga anasuta wanafunzi kwa kuwa vitegemezi baada ya
mwanafunzi kutaka kueleza namna fasihi inaelekeza.
b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hili (alama 2)
Tashbihi- Si kama watoto wakembe
c) Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua (alama14)
Dennis Machora na wanafunzi wenzake wanangojea Dkt Mabonga amjibu mwanafunzi ili nao wapate kujua
Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu wanapiga ubwete na kugeuka kupe.Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu hatafuti chakula.Wanafunzi wengine wanaonelea waache masomo waende kusimamia biashara za wazazi wao.Msichana mmoja alisema kwamba
mchumba wake ni katibu katika wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia, kwa hivyo karibuni watafunga ndoa aondokewe na adha ya masomo.Penina alikuwa anatumiwa shilingi elfu tano kila wiki na wazazi kwa matumishi. Aidha Dennis Machora alikuwa anategemea makupo wa shule kujihikimu. Pesa hizo zinapoisha anahangaika.Dennis Machora aliona kuwa Penina angekuja
kulalamika kuwa Dennis Machora amekuwa kupe.Penina alisema kuwa hangeweza kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa.


|