Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Huku ukirejelea hadithi za “Tumbo Lisiloshiba” na “Shibe Inatumaliza”, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki.

 (5m 56s)
18358 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Huku ukirejelea hadithi za “Tumbo Lisiloshiba” na “Shibe Inatumaliza”, fafanua maudhui ya ukiukaji wa haki. (al.20)
TUMBO LISILOSHIBA.
Viongozi kuweka vitego na vikwazo vya sheria ili watu wadogo wasiweze kutetea mali zao. Kutowahusisha maskini katika maamuzi muhimu yanayoathiri maisha yao. Kunyakua ardhi ya madongoporomoka ambapo watu maskini
waliishi.Kupanga njama za kuwapatia wanyonge visenti vichache ili waondoke madongoporomoka. Jitu la miraba mine kula chakula chote bila kubakishia wateja.Wanamadongoporomoka kubomolewa vibanda vyao na mabuldoza.
SHIBE INATUMALIZA.
Mzee mambo kulipwa kwa vyeo viwili alivyovifanyia kazi. Waajiriwa kwenda
kazini na kukosa kufanya kazi.Viongozi kuibia wananchi kwa kujipakulia mshahara.Waajiriwa wawili kufanya kazi moja – Sasa na Mbura ni mawaziri wa wizara moja.Mzee mambo kuandaa sherehe ya kuingiza watoto nasari kwa kutumia pesa za umma.Mzee mambo kuandaa sherehe kwa kutumia rasimali za nchi- magari, vyakula.


|