Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.

 (7m 2s)
5310 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.
-Mzee Mambo anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea mishahara kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyi kazi yoyote.
-Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwa
kupanga na kupangilia wapi kwa kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.
-Wananchi wa taifa la Mzee Mambo wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia kwenda kazini bila kujali kama wanafanya kazi yoyote. Muhimu si kwenda kazini ila kufanya kazi.
-Mzee Mambo anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wa
taifa kuandaa sherehe zisizo na msingi wowote. Anaandaa sherehe kubwa kwa madai ya kusheherekea kuingizwa kwa mtoto wake “nasari”.
-Mambo anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake.
-Walaji katika sherehe ya kuingizwa kwa mtoto wa kwanza wa Mzee Mambo nasari wanatumia uhuru wao wa kula vibaya kwa vile
hawachunguzi kile wanachokula.
-Vyombo vya habari vinatumia uhuru wao vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi moja kwa moja, badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.
-Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao wa kula kila kitu kibaya na kizuri, wanachokijua na wasichokijua, vyao na vya wenzao hata vya kuokotwa.
-Dj na wengine wenye nafasi katika taifa wanatumia uhuru wao kupokea mabilioni ya pesa za serikali kutumbuiza katika sherehe za mtu binafsi.
-Dj na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za maji, umeme, matibabu miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakilazimika kulipia huduma hizi kwa dhiki na ufukara.


|