Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

"Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkata wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo hii.(alama 4)
b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.(alama 4)
c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi nzima.(alama 6)
d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo.(alama 6)

 (11m 1s)
7332 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
"Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkata wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
Mzungumzaji ni Penina. Anamzungumzia Dennis Machora.
Wako nyumbani kwao katika mtaa wa New. Zealand.
Dennis Machora alikuwa amerudi nyumbani kutoka kampuni ya kuchapisha
magazeti alikoenda kutafuta kazi lakini akaambulia patupu.
b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
Methali - Mgomba Changaraweni haupandwi
ukamea
Swali balagha - penzi lenu na nani?
Nidaa . . . Mkata wee!
Msemo - potelea mbali.
Mdokezo (.....)
c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
Maudhui ya Utabaka.
Wazazi wa Dennis walijitahidi kumsomesha kwa kuwalimia matajiri mashamba. Wazazi wa Penina walipinga uhusiano wa Dennis na Penina kwa kuwa alitoka tabaka la chini ilhali wao walikuwa matajiri. Dennis anakunywa uji kama chamcha kwa kukosa chakula ilhali
Penina hupokea shilingi elfu tano kila wiki. Dennis hangejiunga na shule aliyoalikwa kwa umaskni ilhali wenzake walisomea shule za hadhi kubwa.Penina anapangiwa nyumba katika mtaa wa New Zealand. wanakoishi watu wenye mapato ya Kadri. Penina anamkataa Dennis kwa kuwa hana uwezo wa kifedha kwa kukosa kazi na hangeweza kudumisha maisha yake ya
kifahari. Wazazi wa Dennis walimtegemea asome ili kuwatoa umaskinini ilhali wazazi wa Penina wanamkimu hata baada ya kumaliza masomo.
d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
Msaliti - Alimsaliti mchumba wake Dennis kwa kumfukuza na kumwaibisha sababu ya umaskini. Mwenye dharau -
alimfokea Dennis kwa dharau akimwita mkata. Mwenye tamaa - ana tamaa ya mapenzi na akatafuta mchumba kwa bidii. Mwenye bidii masomoni – alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha kivukoni. Ni jasiri - alimwendea Dennis kutafata mapenzi na uchumba na mambo yanapokwenda kombo anamfukuza bila woga.
Mpyaro - alimtusi Dennis akimwita mkata


|