Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“Ndugu yangu kula kunatumaliza” “Kunatumaliza au tunakumaliza”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
i) Fafanua maana ya kitamathali katika kauli ‘kula tunakumaliza’ (alama 10)
ii) Kwa mujibu wa hadithi hii, ni kwa namna gani wasemaji wanadai kula kunawamaliza? (alama 6)

 (7m 14s)
5809 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Ndugu yangu kula kunatumaliza”
“Kunatumaliza au tunakumaliza”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
-Kauli ya kwanza ni ya mbura
-Kauli ya apili ni ya sasa.
-Walikuwa nyumbani kwa Mzee Mambo
-Mzee Mambo alikuwa ameandaa hafla ya kusherekea mtoto wake kusajiliwa kwenye
shule ya nasari na wa pili meno yalikuwa yamepasua ufizi.
-Wanasema haya baada ya kula sana kwenye sherehe hiyo.
i) Fafanua maana ya kitamathali katika kauli ‘kula tunakumaliza’ (alama 10)
-Mzee Mambo kuwa waziri kivuli wa wizara zote –
anapokea mshahara lakini hana kazi yoyote.
-Wafanyikazi ni watepetevu-wanafika kazini lakini hafanyi lolote pale kazini.
-Vyeo vya mzee Mmambo vinampa fursa ya kupakuwa mshahara.
-Mzee mambo kuandaa sherehe kubwa ambayo inaangaziwa na vyombo vya habari.
-Wizara moja inaendeshwa na mawaziri wawili – Sasa na
Mbura wanadai kuwa wao ni mawaziri wa wizara ya Mipango na mipangilio.
-Sasa na Mbura kuendesha wizara kwa namna ya kujifaidi. Wanasema wizara inawaendesha hasa. Uk 37.
-Magari ya serikali kutumiwa vibaya kwenye sherehe ya Mzee Mambo kuleta jamaa zake, kuleta sherehe havipikwi hapo bali vinaagizwa kwa mali ya umma. Uk 39.
-Mbweo anayoitoa Mbura (uk 40) ni ishara ya shibe aliyonayo. Hizi ni dalili za majitapo/kiburi cha viongozi kuridhika na hali yao ya kuendelea kufaidi kwa wizi.
-Maelezo ya jinsi Sasa na Mbra wanafakamia chakula upsei yanatupa taswira ya jinsi wenye uwezo wanapapia mali ya umma bila kuona haya.
ii) Kwa mujibu wa hadithi hii, ni kwa namna gani
wasemaji wanadai kula kunawamaliza? (alama 6)
-Magonjwa yanayosababishwa na kula lishe isiyobora mfano sukari, presha, saratani, obesti n.k
-Kuna mauaji- watu wanauana kwa kutumia silaha za maangamizi kama vile risasi na mabomu au hata kunyongana kutokana na unyakuzi wa mali ya umma.
-Kuna hai ya kuuna kifikira na kimawazo.
-Uhalifu wa kunyang’anyana mali.
-Kutokuwa na utu/ukosefu wa heshima.


|