Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Bara la Afrika limekumbwa na umaskini mkubwa. Fafanua dhana ukirejelea hadithi ya “Tumbo lisiloshiba” na “Mapenzi ya Kifaurongo”

 (5m 46s)
9254 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Bara la Afrika limekumbwa na umaskini mkubwa. Fafanua dhana ukirejelea hadithi ya “Tumbo lisiloshiba” na “Mapenzi ya Kifaurongo” (alama 20)
TUMBO LISILOSHIBA
Eneo la Madongoporomoka ndiko wanamoishi watu wepesi wasio na mashiko.Watu wa Madongoporomoka walikuwa maskini.Katika eneo la Madongoporomoka kulikuwa
na mkahawa mshenzi wa Mzee Mago.Bi Suruti alishangaa kwa kuuliza kuhusu wanachojali matajiri kuhusu maskini kama wao.Huko Madongoporomoka kuna mashonde ya vinyesi, vibwagizo wa choo, uchafu unaonekenya, vibanda uchwara na maji chafu
MAPENZI YA KIFAURONGO
Dennis Machora alisema kuwa umaskini uhostakimu kwao
haukuwa na mfano.Dennis Machora alisema kuwa wazazi wake hawakuwa na mali ya kuwarithisha.Dennis Machora hana chakula, inabidi apike uji usiokuwa na sukari.Dennis Machora alikuwa na kijiredio na ametandika kitandani shuka zilizozeeka na kuchanikachanika.Penina alimwangalia msimulizi kwa huzuni yamkini alitelewa na hali yake duni.Dennis Machora alimwambia Penina kuwa
hawawezi kuwa na usuhuba kwa kuwa Dennis anatoka kutoka familia ya umaskini naye Penina anatoka kwenye familia yenye nafasi.


|