Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili (alama2)
c) Fafanua sifa za msemaji (alama 4)
d) Jadili maudhui ya utabaka ukirejelea hadithi husika. (alama 10)

 (7m 13s)
3312 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani. Mzoea vya sahani, vya vigae haviwezii”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
Msemaji ni dennis akimwambia Penina wakiwa chumbani mwa Dennis katika chuo. Penina alikuwa anamwelezea Dennis kuwa angetaka awe mpenzi wake ndipo Dennis anapinga kwani wanatoka matabaka tofauti
b) Taja tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili (alama2)
Msemo- tunapigania mikono ilekee vinywani
methali – mzoea vya sahani vya vigae hawezi
c) Fafanua sifa za msemaji (alama 4)
Sifa za Dennis
- Msomi
- Mwenye bidii
- Mwepesi wa kushawishika
- Mwenye majuto
- Mwenye wasiwasi
- Limbukani wa mapenzi
Mpweke
d) Jadili maudhui ya utabaka ukirejelea hadithi husika. (alama 10)
-Matajiri wanaendesha magari ya kifahari
-Wazazi wa Dennis ni maskini
-Wazazi wa Dennis wanafanya kazi ya vibarua
-Dennis alikosa chakula akanywa uji
-Penina alitumiwa shilingi elfu tano kila wiki za matumizi.
-Wazazi wa wanafunzi wengine walimiliki mabasi na matatu hivyo ni matajiri
-Wengine walimiliki nyumba za ghorofa
-Wanafunzi wengine walimiliki simu za dhamani
-Wengine walivalia mavazi ya vitambaa vya dhamani na vilivyovutia
-Watoto wa maskini hawakufanya vyema katika mitihani yao
-Dennis alikuwa bila mpenzi kwani vijana maskini hawakupendwa
-Shakila alitoka kwenye familia tajiri ambapo wazaziwe walimiliki shirika la uchapishaji.


|