Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla Ali)

Maudhui katika hadithi fupi Ndoto ya Mashaka-Ali Abdullah Ali

 (6m 55s)
7259 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Maudhui katika hadithi fupi “Ndoto ya Mashaka”-Ali Abdullah Ali
(a) Mkosi maishani
-Mashaka alikuwa na mkosi tangu alipozaliwa. Wazazi wote walifariki akiwa mchanga. Alipata mlezi ambaye alikuwa fukara. Mashaka aliishi kwa kufanya vibarua ili kumsaidia
-Biti Kidebe mlezi wake. Alipomaliza tu chumba cha
nane mama mlezi akafariki. Mashaka anaoa binti mrembo lakini kutokana na ufukara anamkimbia yeye na watoto saba.
(b) Utabaka
Mwandishi anaangazia suala la utabaka. Anadhihirisha kuwa kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao bado hawajawahi kujinasua. Mwandishi anatoa tathmini
pana ya chanzo cha umaskini. Anaonyesha kuwa katika mtaa wake wamo maskini wengi.
Chumba cha Mashaka kwa mfano kimepakana na cha jirani. Maji ya kuogea yanapita karibu na chumba cha chao. Watu wanaoishi katika mandhari haya ni maskini wa kupindukia.
(c) Ukombozi na mabadiliko
Wasakatonge wanaona kuwa, hali zao zinakatisha tamaa.
Wanapanga maandamano ili kujikomboa. Waliandamana huku wanapiga kelele "Tunataka tufe! Bora tufe! Walifikia kauli hii kwa sababu walichoka kusubiri. Waandamanaji wanazidisha kelele.


|