Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla Ali)

Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya Ndoto ya Mashaka

 (10m 32s)
4721 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu katika hadithi fupi ya “Ndoto ya Mashaka”
(a) Kuna matumizi ya nyimbo
-Wimbo wa kwanza ni wimbo wa kuhimiza watu wathamani na kula aina duni ya ndizi ambayo inaweza kufaa ikipata mpishi bora. Wimbo wa pili, umenakiliwa kutoka Redio Tanzania. Huu unatumiwa kuonyesha kuwa Waridi alipomwimbia mumewe Mashaka alikuwa
anampa kidokezo kuwa anaondoka kurejea kwa wazazi wake.
(b) Methali
-Baada ya dhiki faraja
-Apewaye ndiye aongezwaye
-Kitanda usichokilalia huwajui kunguni wake
-Jungu kuu halikosi ukoko
-Siri ya mtungi iulize kata
(c) Tanakali za sauti
-Kokoko iikoo
-Kwa kwaa
-Puu ngwaaa
(d) Kinaya
Mzee Rubeya tajiri mtajika wa ukoo wa Mwinyi anamuo bintiye kwa kijana hohehahe.
(e)Takriri
Miguu hiyo mie nitaingia nayo kaburini! Ee miguu gani hii.
(f) Jazanda
-Kibuyu hakifichi mbegu.
-Mashaka anarejelea vile ambavyo siri hazifichiki.
(g) Taswira
-Kuna taswira ya wanyonge wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa kwa wino uliokoleza
-Kifafa cha uzazi kilimpiga dafrau akaanguka chini.
-Picha ya mama Mashaka ya kufa ghafla.
(h) Tashihisi
-Rangi ya urujuani ilichungulia katika nyufa
-Kitanda changu cha mayowe kikapiga ukulele.
(i) Tashbihi
-Zimepotea bilashi kama moshi
-kufuriana kama unga uliomwagiwa hamira
(j) Ndoto
Baada ya Waridi kumkimbia Mashaka aliota ndoto, kwamba wanyonge waliandamana wakadai haki zao kwa nguvu, Walisubiri lakini hawakufaulu. Wakaanza tena harakati zao.
Wakati huu wakawa wana hasira zaidi na wakazidisha kelele. Pia wakabeba mabango yenye ujumbe mkali zaidi.
Mabadiliko yakaanza, na wanyonge wakapata maisha bora.


|