Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla Ali)

Muundo wa hadithi Ndoto ya Mashaka-Ali Abdullah Ali

 (6m 31s)
2587 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Muundo wa hadithi “Ndoto ya Mashaka”-Ali Abdullah Ali
-Hadithi hii ina muundo usio sahili. Kuna sehemu zilizogawanywa kwa vinyota. Kila sehemu inabeba maelezo tofauti. Sehemu ya kwanza inaeleza juu ya Waridi binadamu na waridi ua wakati huo huo.
-Katika msuko wa maelezo hayo ameelezea sifa za waridi ua na Waridi binadamu yaani mkewe.
-Sehemu hiyo pia inakuwa kama muhtasari wa kisa kizima.
-Baada ya kitangulizi hicho msimulizi anaelezea kisa kilichokuwa kimetokea kabla ya sehemu hiyo ya kwanza, iliyotengwa kwa kinyota. Hapa anaeleza usuli wake na mikasa yote iliyomsibu.
- Sehemu inayofuatia kwa mtiririko mmoja, inaelezea juu ya ndoa yake ya mkeka.
-Baada ya nyota anaelezea maisha ya ndoa yao.
- Hadi sehemu inayoonyesha maisha ya ndoa. Usimulizi wa mkewe alivyomkimbia na mashaka yaliyompata unafuata.
Sehemu ya mwisho ina kitangulizi au anwani isemayo; 'Siku nyingi tena ' Sehemu hiyo inaonyesha ndoto na mawazo yake aliyokuwa nayo.Ploti ya aina hii huitwa ploti changamano.


|