Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla Ali)

Mhusika Mashaka na sifa zake katika hadithi “Ndoto ya Mashaka”

 (5m 30s)
4204 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mhusika Mashaka katika hadithi “Ndoto ya Mashaka”
Kama lilivyo jina lake alikuwa na maisha ya mashaka. Ni yatima aliyelelewa na Biti Kidebe mwenye roho nzuri lakini mnyonge.
Sifa za Mashaka
Alikuwa na bidii: alifanya vibarua vya kila namna
kumkimu binti Kidebe mama mlezi.
-Ni maskini: alizaliwa katika ufukara na juhudi zake za kujitoa hazikufua dafu.
-Ana mapenzi ya dhati: aliwapenda watoto na mke wake, wanapomkimbia anasononeka.
-Mwota ndoto: mawazo yake na subira kuhusu kujinasua
kutoka makucha ya ufukara yanamfanya daima aote ndoto.
-Ana nyota ya jaha: alibahatika kupendana na binti mkwasi na wakafungishwa ndoa. Hata hivyo familia hiyo haikuwa saidia wakaendelea kusalia katika ulitima.
-Mwenye majuto: anajutia hali yake ya ufukara na kutamani angeweza kupata suluhisho la kudumu.


|