Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Mapenzi Ya Kifaurongo (Kenna Wasike)

Mbinu za lugha katika hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo

 (13m 2s)
4986 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu katika hadithi ya “Mapenzi ya Kifaurongo”
Taharuki
-Kuna taharuki, wakati mlango wa Dennis unapogongwa: Mja huyo ni nani, Penina alijuaje kuwa huyu kijana anaitwa Dennis.
-Wakati kisa kinapomalizikia pia kuna taharuki: Je Dennis alienda wapi? Alipata mastakimu vipi bila fedha?
Penina aliendelea kuishi katika nyumba ile.
Balagha-mbinu ya maswali yasiyohitaji jibu moja kwa moja
-Wavulana wangapi wamejikuta wakining'inia bila kupenda kwao'?
-Kwani swali langu liko vipi? Kwa nini wanafunzi anacheka? Maswali haya
yanamhusu Dennis. Kwa nini ninalia sasa
-Fukara aliyefukarika mpaka mwisho aseme nini mbele ya wanaojigamba na kujishaua?
Tashbihi-ulinganisho usio wa moja kwa moja
-Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi
-Nimetoka ofisini kama mgonjwa mahututi.
-Nimeweweseka kama ubua
-Mapenzi ni matamu kama uki.Yametengana kama ardhi na mbingu
Methali
-Mzoea sahani vya kigae haviwezi
-Ujapokosa la mama hata la mbwa huanwa
-Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura
-Mtu huvuna alichopanda
Misemo
-Hazipunguzi hazizidishi
Utabiri-mbinu ya kubashiri mambo kabla ya kutokea
-Dennis alitabiri vile ambavyo Penina alimpenda wakati huo" akasema kesho anaweza kuwa chanzo cha kero na usumbufu. Huba
litakuwa limekufa na kufukiwa kaburini.
-Hili lilitokea baada ya kukaa kwa miaka miwili na mchumbake Penina.
Litifai-huu ni unukuzi wa makala mengine
Kuna maneno yaliyodondolewa katika riwaya ya utengano "Na nyumba hii uione paa"
Kuchanganya ndimi
-Your competence is doubtful,
-Tarmacking
Mjadala wa nafsi/uzungumzi nafsia
-Dennis anapofukuzwa anajizungumzia sijui kama mimi ndiye kupe au mlazadamu.


|