Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Mame Bakari (Mohammed Khelef Ghassany)

Mhusika Bakari na sifa zake katika hadithi Mame Bakari

 (7m 38s)
2259 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mhusika Bakari katika hadithi “Mame Bakari”
-Huyu ni baba yake Sara.
Sifa zake
-Anaonyesha kuwa ni mtu mkali maana binti yake anashindwa na kumweleza tukio la kubakwa shuleni.
-Baadae anabadilika na kuwa mpole akampatia matunzo mtoto wake.
-Ni mcha Mungu: anafanya sherehe ya Maulidi baada ya mame Bakari kuzaliwa.
-Ana mlahaka mwema na majirani: anawakaribisha watu wote wakiwemo majirani kusherehekea kuzaliwa kwa Mame Bakari.
-Ni mfariji: anamfariji mwanawe na kumpoza wakati alipoangua kilio katika chumba cha daktari.
-Mwenye mapenzi ya dhati: baada ya kugundua kuwa Sara ana himila alimheshimu na kumwita mama.
-Ni msiri: ingawaje walifahamishwa hali ya Sara mapema na mkewe, waliiweka siri na hawakuonyesha kama walifahamu chochote hadi siku rasmi iliyopangwa.
Umuhimu wa Bakari katika hadithi fupi “Mame Bakari”
-Kutoa msaada kwa wanaodhulumiwa. Aidha, ni kielelezo cha wazazi ambao wako tayari kubadilisha msimamo mkali wa ulezi na kutoa msaada unapohitajika.
-Anawakilisha umuhimu wa kushirikiana katika malezi kwa wazazi wote wawili.
-Anaonyesha heshima kitandani kwa wanawake wajawazito hata akawa hajaolewa.


|