Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Mame Bakari (Mohammed Khelef Ghassany)

Maudhui makuu katika hadithi fupi, Mame Bakari-Mohammed Khelef Ghassany

 (8m 27s)
9852 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Maudhui makuu katika hadithi fupi, “Mame Bakari”-Mohammed Khelef Ghassany
(a) Siri
- Mtu anapopatwa na shida nzito huhitaji kuiweka siri hadi wakati mwafaka. Sarina alitunza Siri ya Sara kwamba ni mja mzito. Aidha walipomweleza Beluwa naye aliahidi kuiweka Siri. Daktari Beluwa aliweka siri lakini akawa ametafuta dawa bora
Zaidi ya kuwaeleza wazazi wao.
(b) Uhalifu
Yule nduli ambaye ndiye baba mtoto wa Sara, alitenda tendo la kinyama kwa msichana. Msichana mnyonge na dhaifu, alijaribu kupigana nalo likamshinda nguvu. Hata hivyo uhalifu haulipi chochote. Alimdhulumu Sara na kutoroka akamwacha
amezirai nusu uchi. Unyama huo unafikia mwisho wakati alipojaribu kubaka msichana mwingine.Aliadhibiwa vikali akaupoteza uhai wake.
(c) Kifo
Kuna kifo ambapo janadume lililombaka Sara linauliwa karibu na pao. Sara mwanzoni pia anapania kukiavya kitoto chake.
(d) Malezi
Wazazi wake Sara wanamlea kwa penzi licha ya tatizo lililompata la kubakwa na kupata mimba mapema.
(e) Elimu
Twapashwa kwamba Sara alikuwa msomi aliyebakwa akienda masomo ya ziada.


|