Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Masharti ya Kisasa (Alifa Chokocho)

Mhusika Kidawa na sifa zake katika hadithi Masharti ya Kisasa-Alifa Chokocho

 (4m 47s)
3798 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mhusika Kidawa katika hadithi “Masharti ya Kisasa”-Alifa Chokocho
Mwanamke mrembo ambaye alitaka kuolewa na wanaume wengi. Aliwakataa na kuwachuja hadi akamchagua Dadi. Yeye alisoma hadi kidato cha nne.
Sifa za Kidawa
Ni mzingatifu: anajua alitaka nini maishani na akazingatia matakwa yake ya ndoa ya kisasa.
Alithamini ndoa yake: ili kuiauni ndoa yake anaamua kwenda kujiuzulu kazi ya umetroni pale kazini.
Ni mwenye bidii: Anaifanya kazi ya ziada pale mtaani wakati hayupo kazini ili kuikimu familia yake na Dadi.
Ni jasiri: mwacha mila ni jasiri. Hakuyumbishwa na umbeya wa wanajamii kama Dadi bali aliendelea kuishughulikia familia yake.


|