Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Masharti ya Kisasa (Alifa Chokocho)

Maudhui katika hadithi fupi masharti ya kisasa

 (13m 14s)
8982 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Maudhui katika hadithi fupi “masharti ya kisasa”-Alifa Chokocho
(a) Migogoro ya wanandoa
-Kidawa alijua mabadiliko yaliyomo maishani. Ingawa wanaume wengi walimtaka yeye aliahiri yule atakayefuata masharti yake. Alimtaka Dadi atoe uamuzi. Dadi alitoa uamuzi bila kuelewa kwa undani. Kutokana na hayo kukaingia
kutoaminiana. Ukale aliokuwa nao Dadi, na desturi za kitamaduni zikaleta mgongano. Laiti angalijua
(b) Ahadi maishani
-Kidawa alijua anataka maisha ya aina gani na akafanya uamuzi wake. Aliamua kuwa mume atakayemuoa afuate masharti ya kisasa. Dadi anapewa masharti na ayakubali. Alijitahidi sana kuyashikilia
kwa miaka tisa. Hata akakubali kwamba wapate mtoto mmoja kufuatilia usasa. Kwa Dadi hakuyaelewa yale masharti vyema baadae yanamletea karaha na maisha yake yakavia.
(c) Elimu
-Elimu ni muhimu maishani. Kutokana na mwanga wa elimu mtu husika anapata maarifa na ujuzi wa kupanga maisha yake. Kidawa
alimaliza kidato cha nne na akatumia ujuzi wake kuandaa maisha.
-Kutokana na elimu duni ya Dadi, anaingiwa na shaka na kumshuku mkewe. Akaona kwamba japo hajasoma, amebaini kuwa Kidawa anamwendea kinyume.
(d) Urembo
-Mwanamke akivaa vizuri asichukuliwe kwamba ana macho ya nje. Kidawa alipenda kudumisha urembo wake. Dadi akamdhania anamvalia mwalimu mkuu. Kidawa alijimudu kwa ajili ya biashara ya uchuuzi alitembeza bidhaa zake. Hayo yote Dadi aliyaelewa vibaya na vikamzidishia hofu isiyokuwa ya msingi.
(e)Umbea na masengenyo
-Dadi alihofia minong'ono ya watu ambao walikuwa wanamsema kwa vile alisaidiana na mkewe. Jambo hilo likamnyima raha. Wanawake na wanaume walimsema kuwa alidhibitiwa na Kidawa. Jambo hilo linamwumiza mno.
(f) Mapenzi ya dhati
-Dadi alimpenda mno Kidawa, hata alipopewa
masharti ya kisasa Pindi wakioana aliyakubali bila kufikiria kwa makini maneno hayo baada ya miaka tisa anashindwa kushikilia masharti, akajiumiza bure bilashi akitafuta ithibati.


|