Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Form 2 Kiswahili End of Term 2 Exams 2021

Class: Form 2

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 2 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1619     Downloads: 45

Exam Summary


MWISHO WA MUHULA WA PILI, 2021
KISWAHILI
KIDATO CHA PILI


JINA ----------------------------------------------------------- NAMBA _____DARASA _______
MUDA: SAA 2
ALAMA: 70
1. INSHA (AL 20)
ANDIKA INSHA YENYE MANENO YASIYOPUNGUA MIA 400 INAYOAFIKI METHALI ‘MCHUMIA JUANI HULIA KIVULINI’

2. UFAHAMU
FUNGUA SESAME
Jina la Nimrod lilipotea mara tualipoanza kufanya kazi jijini Nairobi. Marafiki na jamaa zake waliamini kuwa alikuwa ameajiriwa huko mjini ingawa hakuna aliyeijua kazi yenyewe vizuri. Hata hivyo waliamini kuwa lazima alikuwa na kibonge cha kazi kwa sababu alivalia kinadhifu na kuishi maisha ya starehe. Tena yeye mwenyewe alikazania kusema kuwa amejiriwa kazi ya maana. Marafiki zake walimfahamu kama “Bwana Sesame”. Mtu wa kwanza aliyempa jina hilo alisema alipendezwa na ujuzi na maarifa yake. “huyu hakosi ufumbuzi wa tatizo lolote. Ni kama ule mlango wa kisa cha Ali Baba na Wezi arobaini. Ukisema ‘fungua Sesame’ unafungu katu,” alisema mtu huyo.

Jamaa walioishi naye katika mtaa wa Urumo walishangazwa na utaratibu wake wa kazi. Mchana kutwa alishinda chumbani mwake. Mara nyingi utamkuta ametulia akitazama runinga yake ndogo. Wakati mwingine atakuwa akifanya kazi yake ndogo ndogo huku akipiga mluzi bubu, ambao haukusikika vizuri. Wakati mwingine atakuwa akiusikiliza muziki kwenye chombo chake cha muziki kilichotingisha jingo zima kutokana na sauti yake nene.

Kwa kawaida alitoka chumbani jioni. Waliomjua walimchangamkia kutokana na uchangamfu wake. Alipenda sana mizaha. Waliopenda kupiga soga walivutiwa na maongezi yake hasa kuhusiana na magari. Aliyajua magari mengi. Mimi naweza kuijua aina ya gari kwa kuusikiliza mlio wake tu”, alisema kila wakati. “wacha kutuvungavunga Bwana wee, haiwezekani !” atasema mwingine. “nini? Unajua mimi ndiye Bwana Sesame mwenyewe!” atasema, halafu wote wataangua kicheko.
Ilifika wakati kampuni kadha zilipoamua kuwapunguza wafanyakazi wake kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Lakini Bwana Sesame hakuwa mmoja wa hao. Hali yake ilibakia vile vile. Aliendelea kuvalia kinadhifu na kuishi maisha yake ya fawaishi. Wakati wenzake wanalalamikia hali ngumu ya maisha, Bwana Sesame hakuwa na lolote la kumsumbua. Aliendelea kukaa bila kazi wala bazi. Lakini watu walitambua kuwa alikua na mazoea yakutoka chumbani majira ya jioni. Hakuna aliyejua alirejea lini.
Sikumoja Bwana Sesame alitoka jioni kama kawaida na kuelekea kwenye shughuli zake za kawaida. Siku hiyo jamaa mmoja wa mtaani alikumbana naye kwenye lango kuu. “Bwana Sesame,leo wapi yahe?alimwuliza. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “natoka nje kidogo yahe. Jiji hili lataka ustaarabu,’ alijibu. Yule jamaa alimwangalia na kumwabia, “nina shida kidogo, sijui kama utanifaa mwenzangu. Wajua tena hali zenyewe siku hizi,” alisema. Nini tena?’ aliuliza Bwana Sesame.
“Nina gari langu ambalo halina redio. Natafuta moja ya bei nafuu…. Kitu kama sony hivi,” alisema. Bwana Sesame alimwangalia na kusema, “hiyo kazi nyepesi kwangu yahe, papai kwa kijiko!” alisema Bwana Sesame akicheka. Jamaa Yule alishukuru na wakaagana.
Bwana Sesame alishika njia kuelekea sehemu zake za kawaida majira kama haya.Naye Yule jamaaa kapinda kama anaangalia mtaani, lakini baada ya muda akageuka na kuamua kumfuata Bwana Sesame.
Bwana Sesame alishika tariki mpaka sehemu ya mazoea. Yule jamaa alimfuata kwambali na mwendo wa paka. Alimwona Bwana Sesame akiingia mahali palipokuwa na banda kuukuu. Muda si muda alitoka na jamaa wengine wakiwa wamevalia maguo ya ajabu. Yule jamaa aliwafuata hadi mahali palipokuwa na ujia mwembamba ulioachana na barabara kuu. Alijificha mahali, na kutokana nahali ya sehemu ile akawa haonekani.
Muda si muda palitokeza gari dogolililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja. Bwana Sesame na wenzake walitokeza na kutupa gogo lililomzuia Yule mwanamke.
Ghafla bin vuu walimvamia; wakaifungua milango ya gari mbio na kujivurumisha ndani. Gari lilitimuliwa kama risasi kuelekea upande wa pili. Wakati huo Yule jamaa ashaliangalia gari lenyewe na kuzihifadhi nambari zake. Alishika njia kurudi zake chumbani.
Siku iliyofuata huyo jamaa hakuwa kazini. Alipokuwa akifungua kinywa alisikia sauti ya kugongwa kwa mlango. Aliinuka na kwenda kuufungua. Bwana Sesame aliingia ndani. “vipi yahe? Hujenda kazini leo? Au umelala sana Bwana?’ alisema Bwana Sesame kwa uchangamfu wake. Muda si muda alimwonyesha redio ya gari aliyokuwa nayo. “umeipata mara moja hii kumbe?’ aliuliza Yule jamaa. “si nilikwambia yahe! Mimi ndiyeBwana Sesame mwenyewe. Hii kwangu si kazi. Ninafahamiana na jamaa wengi wanaoifanya kazi hii,” alisema Bwana Sesame. “naona kweli. Ehh Bwana we! Ndipo waswahili wakasema,ukitaka kuvua vua na wavuvi! Alisema Yule jamaa. “ni kweli kabisa!’” alijibu Bwana Sesame huku akicheka kwa furaha.
Yule jamaa alisimama kuelekea chumbani. Bwana Sesame alitulia akisubiri kupokea ujira wake. Muda mfupi ulipita, kasha mlango wa nyumba ukagongwa. “yahe Bwana, kunagogwa huku!” Bwana Sesame akasema. Yule jamaa alitoka chumbani na kuelekea mlangoni. Mlango ulipofunguliwa waliingia askari polisi wawili. Bwana Sesame hakuwa na upenyu wakutokea. Alitiwa mikononi.Hakujua kumbe Yule jamaa alikuwa kachero. Hapakuwa na ujanja tena. Siku hiyo pwagu alipata pwaguzi. Fungua Sesame haikufaa tena.



Maswali
1. Kwa nini Nimrod alibatizwa ‘Bwana Sesame’? (al 1)


2. Kwa nini watu walioishi mtaani Urumo walishangazwa na utaratibu wa kazi wa Bwana Sesame?(al 2)


3. Unafikiria ni kwanini Bwana Sesame alifahamu sana juu ya magari? (al 1)



4. Je, unafikiri yule jamaa aliagiza aletewe radio alikuwa na haja sana na kifaa hicho kama alivyosema? (al 2)


5. Bwana Sesame alikuwa kachero. Unakubali? Toa maelezo? (al 2)


6.Yule jamaa alipoingia chumbani na kumwancha Bwana Sesame sebuleni unafikiria alikwenda kufanya nini? (al 2)


7. Je, hadithi hii ina mafunzo gani kwako? (al 2)


8. Eleza maana ya misemo ifuaayo kasha itumie katika sentensi (al3)

a) Piga mluzi
b) Piga soga
c) Shika tariki

3. Matumizi ya lugha (al 20)

a) (i) Taja ala sogezi mbili za kutamkia (al 2)



(ii)Tambua sauti yenye sifa zifuatazo (al 1)
konsonanti, kipasuo, ghuna, sauti ya mdomo


b) Tunga sentensi moja na uonyeshe nomino dhahania (al 2)


c) Tambua aina za maneno zilizopigiwa mistari
Mwanafunzi mrefu alienda Nairobi (al1)



d) Bainisha ngeli ya nomino iliyopigiwa mistari. (al 1)
Jeshi la Kenya lilihamisha k ifaru hadi mbuga ya Masai mara.


e) Taja aina mbili za mofimu. (al 2)


f) Taja dhana zinazowakilishwa kisarufi na viambishi vilivyopigwa mistari (al 1)
Walituchezea


g) Bainisha kivumishi katika sentensi hii (al 2)
Matunda mawili yaliuzwa



h) Tunga sentensi ili kubainisha tofauti za kimaana kati ya maneno haya udogo au dongo
(al 2)


i) Kwa kutumia sentensi moja onyesha vitenzi sambamba (al 2)


j) Tunga sentensi moja na uonyeshe kiwakilishi kimilikishi (al 2)


ISIMU JAMII
a) Eleza maana ya istihali zifuatazo za isimu jamii (al 2)
I. Isimu jamii


II. Sajili


b) Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa. Yaeleze yoyote manne (al 8)
i.

ii.

iii.

iv.


FASIHI (AL 10)
Soma shairihilikishaujibumaswaliyanayofuatia

Malenga mlotukuka, kwa tungo zenu teule
Tungo zenye kusifika, zenye nasaha tele
Naomba la uhakika, jawabu enyi wavyele
Wa kuume tangu lini, kuukata wakushoto!

Tangu dahari miaka, mikono ina upole
Meungana pasi shaka, ni miwili vile vile
Mmoja ukisumbuka, mwingine hujaa ndwele
Wa kuume tangu lini, kuukata wa kushoto!

MASWALI
1. a. Shairi hili ni la arudhi. Dhibitisha kwa kutoa sababu tatu (al 3)


b. Nakili kibwagizo cha shairi hili (al 1)


c. Eleza ujumbe mmoja unaojitokeza kwenye shairi (al 2)



2. a. Taja aina zozote mbili za hadithi (al 2)



b. “nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko
i. tambua kipera hiki (al 1)


ii. taja dhima moja ya kipera hiki kijumla (al 1)



 

More Examination Papers