Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Form 3 Paper 2 Kiswahili End of Term 2 Exams 2021

Class: Form 3

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 3 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1206     Downloads: 17

Exam Summary


MITIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI,2021
KIDATO CHA TATU

KISWAHILI
KARATASI YA 2 (102/2)
LUGHA

JINA ………………………………………..NAMBA YA KUSAJILIWA…………………..
JINA LA SHULE ………………………………………DARASA……………………………
Sahihi ya Mtahiniwa............................................................

MUDA SAA 2 ½

MAAGIZO KWA WATAHILIWA

a) Andika jina na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu
b) Jibu maswali yote. Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.

1.PNG


Karatasi hii ina kurasa 9 zilizochapishwa. Wagombea wanapaswa kuangalia ili kuhakikisha kuwa kurasa zote zimechapishwa kama ilivyoonyeshwa na kwamba hakuna maswali yanayokosekana


SEHEMU YA A: UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
“Asubuhi moja ilinipata ndani ya afisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Kilimo. Mwalimu Mkuu, Bi. Tamasha alisikiliza kadhia yangu kwa makini. Hakuonyeha kushtuka kwa yaliyonipata katika umri wangu mdogo hivi.
‘Unaweza kuanza masomo katika darasa la pili. Nitamwomba mzazi mmoja akupe hifadhi,’ alisema Bi. Tamasha. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa maisha yangu katika makao ya wafanyikazi wa mashamba ya chai. Bwana Tenge na mkewe, Kimai, walinichukua kunilea pamoja na watoto wao watano. Wenzangu, nyinyi hamjui adha zinazowapata wafanyakazi wa kima kidogo. Mtajuaje na haamjawahi kukikalia kitanda hiki mkafahamiana a kunguni wake? Ninayowaambia ni asilimia ndogo mno ya niliyoyaona. Chumba cha wafadhili wangu kilikuwa hichohicho kimoja; ndicho cha mlazi, ndicho cha mpokezi, ndicho jikoni. Sebule na chumba cha malazi viligawanywa na shuka moja nyepesi. Usiku sisi watoto tulilala juu ya vigodoro ambavyo ni kama viliwekwa mvunguni mwa kitanda cha wazazi.
“Usiniulize niliyaona na kuyaskia mangapi katika chumba hiki ambacho kiligeuka danguro wakati Bi. Kimai alipokuwa ameenda mashambani. Wakati huu Bwana Tenge angeamua kumleta mwanamke mmoja baada ya mwingine, hapo hapo, mbele ya macho ya wanawe, hadi usiku wa kuamkia siku ya kurudi kwa Bi. Kimai. Mara mojamoja Bi. Kimai angerudi bila kutarajiwana kumshika ugoni mke mwenzake!Mwaa mmoja, miwili, mitatu ... hata nikaona kwamba, mbali na dhiki za kisaikolojia nilizozipata kwa kushuhudia vituko vya kila aina, nilikuwa mzigo mkubwa kwa wahisani wangu. Si kwamba waja hawa walinibagua, la! Kusema hivyo kutakuwa kuwapaka mashizi bure. Hata hivyo nilihisi kwamba nimepata mbavu za kufanya angaa kibarua kidogo, na kuwatua wawili hawa mzigo wa kuninunulia sare na madaftari.
“Nlianza kuchuna majani chai kwa malipo kidogo nikiwa katika darasa la tano. Wakati mwingine ningerauka alfajiri na mapema kufanya kazi kabla ya kwenda shuleni saa kumi na mbili asubuhi. Jioni nilipitia huko huko. Nyakati nyingi nililala humo humo katikati ya michai, wakati mwingine kwa marafiki wanfu, kwa Bwana Tenge, na juu ya uchaga mkubwa wa saruji uliotumiwa kama karo na wauza chakula sokoni. Hakuna mmoja kati ya walimu wangu aliyejua mabadiliko haya hadi pale nilipoufanya mtihani wangu wa darasa la nane na kufuzu vyema.
“Wakati huo Bwana Tenge alikuwa ameishi kupewa uhamisho, akaenda kufanya kazi katika shamba lingine. Ndivyo wafanywavyo wafanyakazi hawa; kuhamishwa kila uchao bila mtu kuwazia kwamba wana watoto wanaoenda shule, na kwamba kuhamahama huku kunawavurugia masomo wana hawa.”

Maswali
i) Eleza namna wazazi wanavyoweza kuchangia katika kuzorotesha maadili ya watoto katika jamii. (al.2)


ii) Onyesha namna haki za watoto zilivyokiukwa katika kifungu. (al.3)


iii) Wafanyakazi wa kima kidogo hupitia dhiki zipi kulingana na kifungu? (al.3)


iv) Eleza sifa tatu za mkewe Tenge – Kimai. (al.3)


v) Eleza namna ndoa inavyosawiriwa katika kifungu. (al.2)


vi) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika kifungu; (al.2)
a. Danguro


b. Kisaikolojia



SEHEMU YA B (ALAMA 15)
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali
Ripoti za kila mara kuhusu uharibifu wa pesa za umma katika serikali za kaunti ni za kusikitisha. Kuna mabilioni ya pesa za mlipa ushuru ambazo hufujwa katika serikali kuu, na hivyo basi wananchi wanakosewa sana wanapoona mtindo huu ukiendelea pia katika serikali za kaunti. Wakati katiba ilipopitishwa mwaka wa 2010, wakenya wengi walikuwa na matumaini mno kwamba ugatuzi ungewatatulia matatizo ambayo walikuwa wakipata katika tawala zilizotangulia, hasa katika maeneo yaliyotengwa kimaendeleo.
Miaka tisa baadaye, kuna mafanikio ambayo yamepatikana ila hatua kubwa zaidi inaweza kupigwa katika kuboresha maisha ya raia kama mianya inayotumiwa kufuja pesa za umma itazibwa. Wizi huu unaojumuisha pia jinsi magavana wanavyobuni nafasi za kazi zisizo na maana ambazo wakati mwingi hupeanwa kwa jamaa na marafiki wao, ni sharti ukomeshwe mara moja.
Kuna wananchi wengi ambao tayari wameanza kufa moyo kuhusu umuhimu wa ugatuzi ilhali ukweli ni kwamba hatungependa kurejelea utawala ulio chini ya serikali kuu pekee. Changamoto za ugatuzi zinazosababishwa na ulafi wa viongozi wachache zinatoa nafasi kwa wakosoaji wa mfumo huu wa uongozi kushawishi wananchi na hata wahisani wasishughulike kuchangia kaatika maendeleo ya kaunti zao.
Juhudi zozote zile za maendeleo haziwezi kufanikisha bila ushirikiano kutoka kwa wananchi na wahisani na hivyo basi ni jukumu la viongozi kuonyesha nia ya kutumia mamlaka waliyopewa kwa manufaa ya raia. Tume ya maadili ya kupambana na ufisadi (EACC) kufikia sasa imeonekana kufanya kazi nzuri kwa kuwasaka na kuwashtaki magavana walio mamlakani na wengine walioondoka, kwa kushukiwa kufuja mali za umma. Tungependa asasi zote zinazohusika na masuala ya kupambana na uhalifu, pamoja na wadau wengine katika jamii wenye nia njema kwa wananchi wasifumbie macho maovu yanayotendwa katika kaunti zetu.
Nchi hii inatawalwa kwa misingi ya kisheria na hivyo basi hakuna sababu kumhurumia kiongozi yeyote anayekiuka sheria anapokuwa mamlakani kwa msingi wa mamlaka aliyoshikilia. Ni kupitia adhabu kali za kisheria pekee ambapo tutafanikiwa kukomesha uongozi mbaya kwani kama wananchi watakuwa wakisubiri kuwaadhibu wahusika kwa kuwaondoa mamlakani pekee, watakuwa wametoa nafasi ya ufujaji kwa viongopzi wapya kila miaka mitano.

Maswali
a. Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno 80. (al.8, 1 ya mtiririko)
Matayarisho



Jibu



b. Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno 70. (al.7, 1 ya mtiririko)
Matayarisho



Jibu



SEHEMU YA C (ALAMA 40)
a. i) Elezea sifa mbili za sauti /e/. (al.1)


ii) Elezea maana ya sauti mwambatano. (al.1)


iii) Onyesha mfano mmoja wa sauti mwambatano. (al.1)


b. i) Elezea maana ya kiimbo. (al.1)


ii) Elezea umuhimu wake. (al.2)


c. Onyesha miundo miwili tofauti ya nomino zipatikanazo katika ngeli ya U-ZI. (Al.1)


d. Bainisha mazingira mawili ambapo alama ya kiulizi (?) hutumika. (al.1)


e. Bainisha aina mbili za silabi katika neno;Alhamisi. (al.2)


f. Yakinisha katika wingi. (al.1)
Mwalimu hakumwadhibu mwanafunzi.


g. Andika sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu. (al.1)
Mtoto analala


h. Onyesha aina mbili za mofimu katika sentensi ifuatayo. (al.2)
Mimi ninasoma vizuri



i. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (al.3)
RN+RT+RN



j. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mishale. (al.3)
Mbaywayu na korongo ni ndege ambao huishi.


k. Bainisha aina za shamirisho. (al.3)
Mwalimu alimwandikia mwanafunzi maagizo kwa kalamu.


l. Bainisha aina ya vishazi katika sentensi. (al.2)
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma amechoka.


m. Andika visawe vya maneno haya. (al.2)
i. Heshima –
ii. Ruhusa -
n. Eleza maana mbili ya fungu hili. (al.2)
Jua lile


o. Onyesha matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika sentensi ifuatayo. (al.2)
Opiyo atakutengenezea mpini wa jembe na kukuletea kwako.


p. Andika sentensi hii upya ukitumia vinyume vya maneno yaliyopigiwa mstari. (al.2)
Mwanafunzi aliketi kisha akakitega kitendawili.


q. Tunga sentensi moja moja ukitumia vitenzi hivi kwa kauli uliyopewa. (al.2)
i. La – (tendeana)
ii. Vaa - (tendwa)


r. Andika kwa msemo wa taarifa. (al.2)
“Tusipofanya kazi yetu kwa bidii na kujitegemea, tutabaki kuwa watumwa katika nchi yetu,” Rais alisema.



s. Tumia ‘O’ rejeshi kama kiwakilishi. (al.1)
Msichana ambaye huja shuleni mwetu ni mwanasheria.


t. Bainisha aina ya virai vilivyopigiwa mstari. (al.2)
Mhadhara huo tata ulitolewa jana jioni.



SEHEMU YA D (ALAMA 10)

a) Taja lahaja zozote nne katika kiswahili. (al.4)


b) Elezea nadharia zozote tatu ambazo huelezea chanzo cha kiswahili. (al.3)


c) Fafanua sifa zozote tatu za salamu katika mazungumzo. Toa sababu tatu.



 

More Examination Papers