Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Form 3 Kiswahili Paper 2 End of Term 3 Examination 2021

Class: Form 3

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 3 End Term 3 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1294     Downloads: 39

Exam Summary


TUTORKE EXAMS
JINA……………………………………… NAMBARI…………... DARASA………………………………

102/2.
KISWAHILI KARATASI YA PILI.
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA TATU 2022
MUDA: SAA 2 ½ .

UFAHAMU.
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea ni suala la chakula. Suala hili linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti. Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe. Uhaba huu unaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu ya uzalishaji wa chakula.
Zaraa katika mataifa mengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua. Kupatikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabia nchini na ulimwenguni. Matendo na amali za watu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na athari asi kwenye tabia ya nchi hiyo. Mabadiliko ya tabia ya nchi huweza kuvyaza ukame kutokana na ngambi ya mvua.
Kibini methali hutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazao mashambani na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizo makubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wachakula. Ili kuzuia uwezekano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na sera za kuhakikisha kuna usalama wa chakula. Kwa mfano, pana haja kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa upande mwingine, sharti zichukuliwe hatua mufti za kuzuia na kupambana na athari za gharika.
Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakula kilicho sibikwa na vijisumu au kwa njia nyingine ile huweza kumdhuru anayehusika. Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan, uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo, kutozingatia mbeko za usafi, uandaaji wa chakula na kukiweka katika hali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua-hali inayochochea ukuaji wa viini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.
Ili kuepuka uwezekano wa kuathirika, pana haja ya kuzingatia usafi wa chakula na uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe safi, kanuni za usafi zifuatwe, upikaji na uandaaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raia wenyewe zitaathirika pakubwa.

Maswali.
(a) Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea. (alama 2)

(b) Taja hatua mbili zinazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula. (alama 2).

(c) Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 4).

(d) Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1).

(e) Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa? (alama 4).

(f) Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumiwa: (alama 2).
(i) Ngambi ya mvua…………………
(ii) Adha………………………………

MUHTASARI.
Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili. Uwazaji huu umekitwa kwenye matumizi ya michakato kama makini, upangiliaji, uteuzi na tathmini. Hata hivyo, uwazaji huu si mchakato mwepesi bali ni mchakato changamano.
Mchakato wa uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti. Mathalan, kuweza kutambua na kubainisha misimamo ya watu wengine, hoja wanazozua na uamuzi waliofikia, kutathmini au kupima ushahidi uliopo ili kubainisha mitazamo tofauti. Vilevile, uwazaji tunduizi hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki pamoja na kutambua yaliyofichwa au ukweli uliofunikwa na taswira ya juujuu. Hali kadhalika, uwazaji tunduizi hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia misimamo Fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi. Aidha, uwazaji huu huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi, kufikia uamuzi kama hoja zinazotumiwa zina mashiko au zinakubalika kuwa nzuri. Zaidi ya hayo, uwazaji tunduizi unahusisha kuwasilisha mtazamo kwa njia yenye uwazaji mzuri inayoshawishi.
Uwazaji tunduizi una manufaa anuwai. Mosi, unasaidia kujenga makini ya utendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe na malengo wazi. Faukayahayo, unamsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katika matini au ujumbe Fulani bila ya kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni. Uwazaji huu unasaidia kuuchonga uwezo na kuikabili au kuiitikia hali Fulani na kukuza stadi za uchanganuzi. Mwanadamu huwa mtu tofauti na bora anapoujenga na kuimarisha uwazaji tunduizi wake.
Maswali.
(a) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwanzo.
(Maneno 70-80) (alama 10; alama 2 za utiririko)
Matayarisho:

Nakala safi:

(b) Andika kwa muhtasari mambo muhimu katika aya ya tatu.
(Maneno 35-40) (alama 5; alama 1 ya utiririko)
Matayarisho:

Nakala safi:

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
(a) Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (alama 2)
(i) Kipasuo ghuna cha mdomoni.

(ii) Irabu ya katichini.

(iii) Kikwamizo sighuna cha kaakaa gumu.

(iv) Nazali ya ufizi.

(b) Bainisha silabi zilizowekewa shadda maneno yafuatayo: (alama 1).
(i) Miamba kofi

(ii) Yatazoleka.

(c) Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani (alama 1).
(i) Ugwe……………………
(ii) Limau…………………
(d) Tambua kiambishi awali na tamati katika neno: (alama 2).
Alalaye

(e) Ainisha vivumishi katika sentensihii (alama 2).
Mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi.

(f) Bainisha mofimu katika neno (alama 3).
Atamnywea.

(g) Ainisha vitenzi katika sentensi (alama 3).
Ndege yu taabani, hata hivyo anajaribu kujinasua.

(h) Eleza maana ya kirai (alama 2).

(i) Ainisha virai vilivyopigiwa mstari (alama 1).
Zana hizi zimeundwa na mafundi wenye ustadi mkubwa.

(j) Tunga sentensi yenye kikundi tenzi chenye muundo ufuatao. (alama 2).
Kitenzi kisaidizi, kitenzikikuu, nomino.

(k) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi tofauti ya kiambishi ‘li’ (alama 2).

(l) Andika sentensi ifuatayo katika hali yakinishi (alama 2).
Askari wasipopiga doria wala kushirikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama (alama 2).

(m) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo (alama 2).
Madebe hayo yatasafirishwa pamoja na nyundo hizi.

(n) Huku ukizingatia dhamira, taja aina tatu za sentensi kasha utoe mfano mmoja mmoja. (alama 3).

(o) Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano (alama 1).
(i) La (tendeana)…………………
(ii) Vaa (tendwa)……………………
(p) Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alama 2).
Watahiniwa hao walisoma maswali yote kwa makini.

(q) Bainisha shamirisho kipozi, kitondo na ala katika sentensi ifuatayo (alama 3).
Kipkemboi alimbebea mwalimu mzigo kwa gari.

(r) Andika visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari (alama 2).
Sahibu yake alishikwa na kisunzi.

(s) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (alama 2).
Ingawa mshahara wake si mkubwa anaikimu familia yake.

(t) Eleza matumizi ya hali za“ ka “ na “ hu” katika sentensi zifuatazo (alama 2).
(i) Balozi huja hapa kila mara.

(ii) Mpishi alipika, akapakua na akagawa chakula.

ISIMU JAMII (ALAMA 10).
Eleza sifa kumi za sajili ya lugha kati ya wataalamu wawili.

 

More Examination Papers