Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Form 1 End of Term 2 Examination 2019

Class: Form 1

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 1 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1087     Downloads: 30

Exam Summary


Kiswahili Form 1 End of Term 2 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


1. UFAHAMU (ALAMA 20)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata:
Hapo zamaniza kale palikuwa na mfalme aliyesifika sana. Sifa zake zilienea karibu na mbali. Zilienea kama moto nyikani msimu wa kiangazi.
Mstahiki Salamwana Salamwene, maana hili ndilo lilikuwa jina lake, alikuwa mtu wa ajabu sana. Asili yake yenyewe ilikuwa kitendawili. Inasemekana mamake alibeba mimba iliyopita miezi tisa. Na kila aliposhangaa alisikia sauti tumboni ikisema. “Mama kuwa na subira, bado ninalainisha lugha yangu”
Baada ya muda mama alipolalamika alisikia, “Mama ninakaribia, ninamalizia kunoa ubongo wangu.”
Halafu siku moja ikanyesha mvua kubwa iliyoandamana na radi. Waliokuwepo wanasema waliona mmweso mkali ulioangaza hata kwenye milima mikubwa. Salamwene akazaliwa. Moja ya sifa zake kubwa ilikuwa hekima na maarifa ya ajabu. Hakuna tatizo la watu wake ambalo alishindwa kulitatua. Watu wakawa wanafunga safari za siku nyingi kutoka mbali kuja kwenye ikulu yake. Wengi walienda kwa shida za dhati lakini wengine walikuja kumjaribu.
Siku moja akaja mfanyabiashara tapeli na maua ya aina akamwambia, “Mstahiki mfalme, mtu wako anataka kuniuzia maua haya kwa vipande vingi vya almasi name nina shaka kuwa moja ni la bandia waweza kuniamulia?” Mfalme hakujibu. Naye inasemekana alipenda zaraa na hivyo alikuwa na miti na mimea iliyozaa maua na kutoa harufu anuwai. Basi akaja nyulu na kutua kwenye ua moja. Mfalme Salamwana akamtambulisha ua halisi.
Muda ukayoyoma huku wahitaji wakiingia ikulu na kutoka. Siku moja akaja Binti mfalme mmoja kutoka nchi ya mbali na msafara mkubwa. Alipokewa kwa taadhima. Alikaa mwezi mmoja. Kila siku alikaa kwenye baraza akishuhudia mfalme akiyatatua matatizo ya watu. Jioni walikaa na mfalme pamoja wapambe wao akijifunza kutoka kwenye hazina kubwa ya busara ya Mstahiki Salamwana.
Usiku uliotangulia kuondoka kwa mgeni, Salamwana alitoa amri za ajabu. Kwanza, aliamuru magudulia yote ya maji kwenye chumba cha kulala mgeni yabadilishwe. Pili, alimwamuru mpishi kupika chakula kilichokolea viungo kutoka Bara Hindi. Tatu, aliwaamuru wapambe kuwa mgeni akiomba chochote wasimpe ila wamfahamishe. Usiku huo, mgeni alihisi kiu kikali lakini aliponyanyua gudulia kumimima maji kwenye bilauri ya dhahabu, halikuwa na maji. Akajaribu la pili, magudulia yote ya shaba yaliyokuwa chumbani hayakuwa na maji. Alijitahidi kuvumilia lakini wapi! Ilibidi atafute msaada kwa wapambe nao wakamweleza walivyoambiwa. Mwanzoni aliona ni kukosa fadhila kumsumbua mwenyeji mwenye staha kama mfalme. Kiu ilipozidi kumkeketa koo alisalimu amri. Mfalme alifahamishwa. Na kama aliyejua alichoitiwa akaja na kigudulia kidogo chenye nakshi ya dhahabu na kifuko cha hariri. Alikuwa radhi kumpa mgeni sharubati ya kukata kiu ila kwa masharti. Anapokunywa maji ameze na zawadi atakayompa ambayo angeitapika afikapo nyumbani.
Keshowe mgeni aliagwa kwa mbwewe na taadhima. Akaanza safari iliyochukua takriban mwezi mmoja. Baada ya miezi kumi, Mstahiki Salamwana Salamwene alipata risala kuwa Binti wa Mfalme alikuwa ameitapika zawadi aliyopewa kama alivyokuwa amekula yamini. Hicho kikawa kitendawili kwa watu wengi. Wakabaki wakiulizana jibu la fumbo hilo.


Maswali
1. Ipe hadithi hii anwani mwafaka. (alama 2)

2. Kwa nini ilisemekana asili ya Mfalme Salamwana ilikuwa kitendawili? (alama 2)

3. Eleza sifa sita za mfalme zinazojitokeza kwenye kifungu.(alama 3)

4. Ni watu gani walikuja kwa mfalme. (alama 3)

 

More Examination Papers