Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Paper 2 Form 3 End of Term 2 Examination 2019

Class: Form 3

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 3 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 867     Downloads: 14

Exam Summary


Kiswahili Paper 2 Form 3 End of Term 2 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


SEHEMU YA A: UFAHAMU (ALAMA 15)
HABARI zisizoridhisha kuhusu shambulizi la kigaidi katika kituo cha biashara cha Westgate, Kaunti ya Nairobi ambapo watu wapatao 67 waliaga dunia na wengine zaidi ya 175 wakaachwa na majeraha, zinaendelea kufichuka. Magazeti yaliangazia habari kwamba mawaziri wanne pamoja na maafisa wakuu wa usalama nchini walipashwa habari za kijasusi kuhusu mipango ya magaidi wa Al-Shabaab kutekeleza shambulizi hilo. Inadaiwa kwamba viongozi hao hawakuchukua hatua za kuzuia shambulizi hilo.

Habari zaidi zilieleza kwamba kituo hicho kilikuwa kinafanyiwa uchunguzi na idara ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) kabla ya kushambuliwa na magaidi. Imeripotiwa kwamba wachunguzaji wa ujasusi walikuwa katika kituo hicho masaa machache kabla ya magaidi hao kufika na kuanza kuwafyatulia risasi walinda usalama, wateja na wafanyabiashara. Inadaiwa wachunguzaji hao 'waliwasiliana' na maafisa wa polisi wanaoshika doria mara kwa mara katika kituo hicho ambacho kimetajwa kuwa miongoni mwa maeneo muhimu sana jijini Nairobi.

Habari hizi zote zinawapa Wakenya ujumbe mmoja; kwamba baadhi ya maafisa wakuu na idara za serikali zilizembea katika majukumu yao ya kuwahakikishia Wakenya na wageni wote wanaozuru Kenya, usalama. Ingawa hatupingi kwamba maafisa hao wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuzembea kazini, jambo muhimu ambalo Wakenya wanataka sasa si lawama bali hakikisho kwamba maisha yao hayapo hatarini wanapoendelea na shughuli zao za kila siku za kuijenga nchi.

Vitisho vilivyotolewa na magaidi hao ambao wamesema wanapanga kutekeleza mashambulizi mengine ndivyo vinavyowakosesha Wakenya Usingizi. Wahenga walisema tusahau yaliyopita na tugange yajayo. Serikali inapaswa kutumia shambulizi la Westgate kama funzo litakalozifanya idara zake za usalama kuamka usingizini na kuhakikisha kwamba Wakenya wasio na hatia hawapotezi tena maisha yao katika mashambulizi kama haya.
Lakini mbona Wakenya nao wasianze kuuthamini usalama wao wenyewe? Hali ya usalama nchini itaimarika maradufu kama Wakenya wote watachakua jukumu la kuwajua vyema majirani wao na kuripoti jambo lolote lisilo la kawaida kwa maafisa wa usalama.

Shambulizi hili lingezuiwa kama Wakenya wangekuwa na mazoea ya kutaka kuwafahamu vyema watu wanaoishi karibu nao kwani inadaiwa kwamba magaidi hawa waliwasili nchini kitambo na kukodisha nyumba ambako waliendeleza mipanga yao. Badala ya kuwalimbikizia lawama polisi, mbona tusishikane nao ili kuhakikisha kwamba watu wenye nia mbaya mitaani mwetu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria?

MASWALI
a. Toa anwani mwafaka kwa taarifa hii. (al. 1)
b. Taja maafa yaliyosababishwa na tukio linalorejelewa. (al. 2)
c. Eleza kinaya kinachojitokeza kuhusu tukio la Westgate. (al.4)
d. Ni nini mtazamo wa mwandishi kuhusuu maafisa wakuu serikalini. (al. 2)

 

More Examination Papers