Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na Majibu Katika Riwaya ya Chozi La Heri

Fafanua namna mwandishi alivyotumia mbinu ya kisengere nyuma katika riwaya (alama 20)

 (7m 40s)
9333 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Fafanua namna mwandishi alivyotumia mbinu ya
kisengere nyuma katika riwaya (alama 20)
Jibu
- Mwandishi huyu amefaulu sana kutumia mbinu hii. Kisengere nyuma imetumika katika mazingira yafuatayo:
- Kisa cha namna Mzee Kedi (jirani yao) alivyomsaidia Ridhaa kupata shamba lake na kuwa ameyadhamini masomo ya wapwaze wawili kimetolewa kwa urejeshi.
- Mijadala baina ya Ridhaa na Tila imetolewa kwa njia ya urejeshi.
- Kisa cha yule mwana wa mlowezi maarufu
aliyemiliki mashamba ya Theluji Nyeusi katika eneo la Kisiwa bora kimetolewa kwa urejeshi.
- Kisa cha yule kiongozi wa Kiimla wa kike aliyekuwa akisimuliwa katika visakale cha majirani zao na namna alivyowatumikisha wanaume kimetolewa kwa urejeshi.
- Kaizari anasimulia yaliyojiri baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya aliyekuwa mwanamke kwa njia ya kurejelea.
- Moyo wa Kaizari ulipoanza kumsuta, alikumbuka kisa cha wafuasi wa Musa ambao baada ya kukosa chakula
jangwani walimshtumu kwa kuwatoa kule Misri.
- Ridhaa alipokuwa ameketi kwenye chumba cha mapokezi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Rubia, alikumbuka namna walivyorudi nyumbani baada ya kuishi katika msitu wa Mamba kwa miezi sita. Anakumbuka pia alivyokuwa akihisi.
- Ridhaa anamkumbuka Tila bintiye alivyokuwa anapenda masuala yanayohusiana na sheria, haki na siasa.
- Mwangeka alipolitazama tabasamu la babake, alihisi kuwa sasa amezingirwa na uzio imara. Akawa anakumbuka wimbo ambao mamake alizoea
kumwimbia kila mara babake alipokuwa ameenda katika safari za kikazi.
- Kisa cha namna Ami zake Kangata walivyokuwa wamekataa mwana wao aolewe na mtu wa ukoo mwingine kimetolewa kwa urejeshi.
- Kisa namna Lunga alivyostaafishwa kwa kuwa na msimamo imara kuhusiana na sakata ya mahindi kimetolewa kwa urejeshi.


|