Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Mbinu za uandishi katika tamthilia ya Kigogo

 (16m 50s)
13634 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu za uandishi katika tamthilia ya Kigogo
(a) Kinaya.
Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya, kuwa wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie ufanisi ambao umepatikana katika kipindi cha miaka tisini baada ya uhuru.
Ujumbe huu ni kinaya kwa vile Sagamoyo hakuna maendeleo wala ufanisi.
Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea. Kauli hii ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile.
Sudi anasema kuwa katika kipindi cha mwezi mzima
wa uhuru wale mali walizochuna kwa miaka sitini. Ni kinaya kwa kuwa hakuna walichovuna, viongozi hujilimbikizia mali.
Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri.Ni kinaya kwa vile hakuna mambo mazuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo.(uk5)
Wanasagamoyo kusheherekea miaka sitini ya
uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusheherekewa, hakuna maendeleo Sagamoyo.
(b) Jazanda.
Kinyago cha shujaa anachochonga Sudi kwamba shujaa huyo nimkubwa kuliko jina lake na urembo wa shujaa huyo ni bora zaidi.Shujaa anayerejelewa hapa ni Tunu,yale ambayo
anatendea Sagamoyo ni makuu kuliko jina lake, kutetea haki za wanyonge.(uk10)
Husda anamwambia Ashua kuwa hawezi kumtoa bonge kinywani hivi hivi.Bonge ni Majoka bwanake Husda kuwa Ashua hawezi kumnyanganya bwana.
Husda kumwita Majoka pwagu, pwagu ni mwizi na Majoka amewaibia wanasagamoyo;ananyakua
ardhi, anaiba kodi na kuwalaghai wanasagamoyo.(uk27)
Husda anamwambia Ashua kuwa ameshindwa kufuga kuku na kanga hatamweza.Kuku ni mumewe Sudi, na Kanga ni Majoka, kwamba Ashua ameshindwa kumtunza Sudi na Majoka hampati.(uk28)
Tunu kuwekewa vidhibitimwendo ni
kukomeshwa au kuwekewa vikwazo ili afe moyo kutetea haki za wanasagamoyo.
(c) Sadfa.
Majoka akiwa ofisini mwake,Ashua anaingia bila kutarajiwa.
Ashua akiwa na Majoka ofisini,Husda anaingia bila kutarajiwa,Ashua anamaka na kubakia kinywa wazi.
Majoka anaposoma gazeti anaona maoni kuwa Tunu awanie uongozi Sagamoyo,hakutarajia kuyaona maoni hayo gazetini.
Chopi wanapozungumza na MajokaMwango anafika na habari kuwa Majoka ana wageni, Tunu na Sudi ambao hakutarajia.
Majoka anapongojea Husda katika hoteli ya kifahari Sagamoyo, Kenga anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga,kuwa Tunu bado yupo, hakuvunjwa miguu, Majoka hatarajii Tunu kuwa mzima.
(d)Wimbo.
-Wimbo wa uzalendo
Wimbo huu unaimbwa katika kituo cha habari cha
wazalendo,ni wimbo unaosifu Sagamoyo na kiongozi wake kuwa;
Sagamoyo ni jimbo tukufu, wanamtukuza Ngao kuwa kiongozi shupavu.
-Wimbo wa hashima
Anaimba wimbo huu akiwa nyumbani kwake.Wimbo huu unaashiria kuwa mambo hubadilika, kila siku wasema heri yalipita jana.(uk51)
-Wimbo wa mama pima
Ni wimbo wa kishairi unaorejela Sudi na Tunu.Mamapima anawashauri wajipe raha kwa kujiunga nao katika ulevi.(uk60)
-Wimbo wa ngurumo
Ngurumo anaimba wimbo kwa mamapima akimrejelea Tunu. Ni wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwanamke anapaswa kuolewa.
-Wimbo wa umati
Umati unaimba wimbo katika lango la soko la chapakazi.Watu wanaimba kuwa yote yanawezekana bila Majoka.Wimbo huu unasifia juhudi za Tunu kuikomboa Sagamoyo na kuleta uhuru halisi.
(e) Ndoto.
Tunu anaotandoto kuwa anafukuzwa na mzee Marara
akitaka mkufu wake wa dhababu.
Mzee marara kumfukuza Tunu ni ishara kumkomesha asiwe kiongozi Sagamoyo (kumnyanganya mkufu), mkufu wa dhahabu ni ishara ya uongozi.(uk53)
Majoka anasema na babu katika ndoto.Babu anamshauri Majoka abadili mienendo yake na asikie vilio vya wanasagamoyo.
(f) Taharuki.
Kombe na Boza wanaagizwa wachonge vinyago, je wanavichonga?
Majoka anampenda sana Ashua, anampata?kama hakumpata, alifanya nini?
Ashua anaomba talaka yake akiwa jela,je anapewa?
Kuna wafungwa ambao wamefungiwa, walifanya kisa gani?je wanaachiliwa? iwapo hawakuachiliwa, hatima yao ilikuwa ipi?
Wageni wanatarajiwa Sagamoyo siku ya uhuru.Je wanafika?


|