Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Mhusika Kenga na sifa zake katika tamthilia ya kigogo

 (4m 42s)
4972 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mhusika Kenga na sifa zake.
Ni mshauri mkuu wa Majoka.
1.Ni mshauri mbaya.
Anamshauri Majoka visivyo.Anamwambia atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha aamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.
2.Ni kikaragosi/Kibaraka
Anamuunga Majoka mkono hata kwa mambo yasiyofaa nia yake ikiwa ni kujinufaisha kutokana na uongozi wake.
3.Ni fisadi.
Yeye na Majoka wanadai kitu kidogo kutoka kwa wanasagamoyo. Baada ya soko kufungwa,Majoka anamwambia kuwa kipande
chake cha ardhi kipo.Anakipata kwa njia isiyo halali.
4.Ni mwoga.
Kenga anahofia maandamano yanayoendelea na kumshauri Majoka asiyapuuze
5.Ni mwenye matumaini.
Hafi moyo, anasema atarudi tena na tena ili kusema na Sudi ili achonge kinyago.


|