Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Matakwa ya wanasagamoyo katika tamthilia ya kigogo

 (6m 36s)
7653 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Matakwa ya wanasagamoyo.
-Soko ambalo ni tegemeo lao linafungwa.Waataka soko lao lifunguliwe na kujengwa upya pia lisafishwe.
-Hawana usalama,askari wanatumiwa kuwatawanya na kuwatishia.Wanaishi kwa hofu.
-Hawana uhuru wa kutangamano kwani viongozi wao wanahofia maandamano.
-Haki zao zimekiukwa.Mauaji yanapangwa kwa njama za kuwaangamiza.
-Wanataka kujengewa hospitali, barabara na vyoo.Waletewe nguvu za umeme.
-Wanataka wapate elimu Sagamoyo na ajira kwa vijana.
-Wanasagamoyo wana njaa
-Walimu na wauguzi Sagamoyo wana mishahara duni.
-Kuna vilio Sagamoyo,mauaji yanapangwa.Wanasagamoyo wanataka mauaji haya yakome na haki kutendwa.
-Wanasagamoyo wananyanyaswa na viongozi, bei ya chakula inapandishwa ilihali wengi wa wananchi ni maskini.
-Mazingira Sagamoyo ni chafu hadi kuhatarisha maisha yao.Wanataka soko kusafishwa.


|