Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tamthilia ya Kigogo (Pauline Kea)

Ufaafu wa anwani ya tamthilia ya Kigogo

 (7m 54s)
8752 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ufaafu wa anwani ya tamthilia ya Kigogo
-Kigogo ni mtu mwenye madaraka makubwa kiutawala.
-Majoka anatumia madaraka yake kulaghai wananchi, anachukua vilivyo vyao.
-Anatangaza kipindi cha mwezi mzima cha kusheherekea uhuru kutumia madaraka aliyonayo.
-Majoka anafunga soko la Chapakazi ili sehemu hiyo ajenge hoteli ya kifahari kwa kutumia madaraka aliyonayo.
-Anapandisha bei ya chakula katika kioskikwa vile ana madaraka.
-Majoka anatumia mamlaka yake kumteka na kumtia ndani Ashua.Anamtendea ukatili, Ashua ana majeraha kutokana na kichapo.
-Majoka anapanga kifo cha Jabali,mpinzani wake.Anampangia ajali na kuangamiza wapinzani wake pamoja na chama chake kwa kutumia mamlaka yake..
-Majoka anapanga kutumia mamlaka yake kuzima uchunguzi wa Tunu kuhusu kifo cha Jabali.
-Majoka anafuja pesa za kusafisha soko huku akijua hakuna wa kumhukumu kwa kuwa ndiye kiongozi.
-Majoka anatumia mamlaka yake kudhibiti vyombo vya habari Sagamoyo,anasema sagamoyo kitabakia kituo kimoja tu cha habari;sauti ya mashujaa, vingine havina uhai.
-Majoka kwa mamlaka yake anaamuru polisi kutawanya waandamanaji.
-Majoka anampa mamapima kibali cha kuuza pombe haramu kwa kutumia mamlaka yake. Kwa mamlaka yake, Majoka anafadhili miradi isiyo muhimu, anafadhili mradi wa kuchonga vinyago kutoka nje.
-Majoka anaamuru wafadhili wa wapinzani kuvunja kambi zao Sagamoyo.Anamfuta Kingi kazi kwa kutomtii apige watu risasi.


|