Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Kidege (Robert Oduori)

Mbinu katika hadithi fupi ya Kidege-Robert Oduori

 (5m 1s)
5602 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu katika hadithi fupi ya “Kidege”-Robert Oduori
(a) Taharuki
-Kuna taharuki ya kujua wapi mapenzi ya Achesa na Joy yameishia. Je, baada ya bustani kuvamiwa na midege waliendelea kuvinjari eneo hilo?
-Kuna taharuki ya kujua kama Mose alifanikiwa kuonana na Shirandula na kumpatia jibu
lake. Kama alimpa jibu, kuna taharuki ya kujua kama jibu hilo lilikuwa sahihi.
(b) Tanakali za sauti, kwa mfano: .shwii shwaa shwii shwaa shwiii.
(c) Misemo na nahau, kwa mfano: binadamu nao na hamsini zao.
(d) Taswira, kwa mfano:
Kidege-huashiria watu wanyonge katika jamii
Midege —Huashiria watu wenye nguvu za kiuchumi/
kiutawala wanaowanyonga wanyonge.
Visamaki — huashiria rasilimali zinazoporwa na watu,nguvu na mamlaka ya kiutawala.


|