Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Tumbo Lisiloshiba (Said A. Mohammed)

Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya Tumbo Lisiloshiba

 (16m 8s)
9109 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya “Tumbo Lisiloshiba”
Taharuki:
-Hadithi inapoanza kuna taharuki. Huo ni uvumi gani? Unazushwa na nani kwa sababu gani? Anaposema haukuwa wa kupasuka bomu au kulipuka mzinga anaendelea kuitilia uzito taharuki hiyo.
-Taharuki nyingine ni ile ya jitu liloingia mkahawa mshenzi lilitokea wapi.Kwa nini liliamua kuutembelea siku hiyo. Je ziara yake ni kula tu chakula au kufanya uchunguzi.
Taswira:
Ni mbinu ya kujenga picha akilini mwa wasomaji.
-Kuna taswira nyingi katika kisa hiki. Kuna taswira ya jitu
la miraba mine kutokana na maelezo ya lile jitu lilivaa suti nyeusi na shati jeupe. Wakati mabuldoza yalipokuwa yakiangusha vibanda na kuwatimua watu. Ni taswira inayoangazia jinsi haki za wanyonge zinavyofifishwa. Aidha jeshi la polisi hushadidia jambo hilo hilo la unyanyasaji wa wanyonge.
Balagha
-Haya ni maswali yasiyohitaji majibu moja kwa moja.
-Mifano: yote hayo lakini yafae nini mbele ya nia ya kuhakikisha nafasi za biashara na malengo ya starehe ya wakubwa
-Chupa mbili za Coca Cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo
Mdokezo:
-Maelezo machache ambayo hayakamiliki, yakitumiwa kuashiria jambo fulani. Lile jitu la miraba minne lilidokeza kwamba kungekuwa na tukio fulani. Kesho kama sote tutaamka salama.
Tashbihi:
-Bweu lilipasuka kama mzinga
-Kiti kilionekana kama cha Shule ya chekechea
Kuchanganya ndimi:
Mbinu ya kuitumia lugha Zaidi ya moja katika kifungu.
-Chauffeur
-AudiQ7
-Coca Cola
-Departmental stores, casinos
Methali –Ni mbinu ya lugha ambapo maneno huwa yamebeba ujumbe wa kina kando na ule unaojitokeza kwa juu juu.
Kuna matumizi ya methali kama kimya kingi kina mshindo
Takriri –Huu ni urudiaji kwa madhumuni ya kusisitiza
-“Hawawezi, hawawezi kabisa hawawezi”
Mbinu rejeshi:
-Uvumi kuhusu kubomolewa kwa vibanda ulianza halafu
ukatoweka. Baadaye uvumi huo unarejelewa tena katika kibanda cha Mzee Mago.
Chuku:
-Ni mbinu ya kutia chumvi katika maneno.
-Ukubwa wa tumbo la mtu mwenye miraba mine limetiliwa.
Chuku:Kwa nini mwandishi amefanya hivi? jinsi
lilivyolamba sahani zote — halikubakisha hata ishara ya chembe moja ya chakula chochote alichokula.


|