Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Tumbo Lisiloshiba (Said A. Mohammed)

Wahusika na sifa zao katika Tumbo Lisiloshiba

 (13m 21s)
21113 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Wahusika na sifa zao katika “Tumbo Lisiloshiba”
(a) Mzee Mago
-Mpenda haki na mtetezi wa haki: yeye hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia suluhisho
-Ni mwenye bidii: shughuli ya kupigania na kuzuia mipango ya watu wakubwa sio rahisi. Ilibidi mzee Mago ajinyime, awatafute wenzake wazungumze na kulijadili jambo hili ambalo lilikuwa nyeti sana kwao.
- Ni mshawishi: aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.
-Ni mzindushi: aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo.
Aliwazindua kwamba maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu wa kike kwa wa kiume, wadogo kwa wakubwa n k. Aidha, aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayowanufaisha.
(b) Kabwe
-Anapenda ushirikiano. Alishirikianana wanyongewenzake katika kutafuta ufumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.
-Anaamini kuwa sheria inaweza kuwa suluhisho la matatizo yao.
-Ni mpenda amani na haki. Alitaka watafute suluhisho linalofaa kwa watu wa Madongoporomoka.
(c) Bi. Suruta
-Ni mshauri
-Ni hodari katika kutoa hoja kwenye mashauriano. Anawapiku wanaume wote.
(d) Bi. Fambo
-Mwanamke mojawapo wa wanyonge.
-Ni mwelewa masuala ya unyanyasaji.
-Anaeleza bayana kwamba wakubwa hawajali wanyonge wakihamishwa kwenye ardhi watakwenda wapi.
(e ) Jitu Ia miraba mine
-Ni mkubwa wa kimo: yeye alikuwa pandikizi la jitu Alipoingia katika mgahawa mshenzi wateja wote waligutuka.
-Ni mlafi: alikula vyakula vyote vya wateja waliokuwepo katika mgahawa wa Mzee Mago na kurudia mara tano kabla ya kushiba. Aidha alikunywa soda nyingi sana. vyakula vyote na hata hakusaza chochote.
-Ni mwenye madaha: Anajishaua na kumwambia Mago kwamba hajakuja kusaidiwa na Mago pale katika mkahawa bali ndiye anamsaidia Mago.
-Ni fisadi: Jitu limehusika katika njama ya kuwaangamiza wanamadongoporomoka na kuwaibia ardhi yao


|