Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Form 2 Kiswahili End of Term 3 Examination 2021

Class: Form 2

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 2 End Term 3 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1861     Downloads: 61

Exam Summary


TUTORKE EXAMS
JINA …………………………………………………NAMBARI …………….DARASA……...

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA TATU 2022
KIDATO CHA PILI
MUDA: SAA 2 ½

MAAGIZO
(a) Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
(b) Jibu maswali yote.
(c) Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
(d) Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
(e) Watahiniwa lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

A. INSHA
Wewe ni mwenyekiti wa kamati ya usalama wilayani mwenu.Andaa hotuba utakayoitoa katika kikao kinachoshughulikia usalama huku ukizingatia chanzo cha tatizo hili na hatua zinazofaa kuchukuliwa kulitatua.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

B. UFAHAMU(alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo.
Wiki iliyopita nilikuwa napanga foleni kuingia kwenye benki nilipopigwa na butwaa.Kilichonistaajabisha ni kuwa dada mmoja alikuwa aking’ang’ania kujibanza mbele pasipo kupanga foleni,bila kuwajali wateja waliokuwa mbele yake.Jambo hilo lilinikera kwani mwanamke hakuwa na wakati wa kuomba radhi kwa waliokuwa mbele yake.
Baada ya kutafakari kwa muda niliamua sitakereka wala kumlaumu kwani ni tabia iliyokita mizizi miongoni mwa wanawake humu nchini.Ni mara ngapi umewaona wanawake wakichukulia wanaume wana muda wote wa kupoteza na kuwakaripia kuwa hawawapi nafasi kwa mujibu wa msemo “ladies first”?Ni wangapi ambao huwanunia na kuwatukana wanaume kwa kuwa hawakutambuliwa wala kuwapa nafasi ya kwanza licha ya kuwa haikuwa haki yao?Ni wangapi huwaaibisha waume wao kwa kukosekana kwa hiki na kile nyumbani licha kuwa wenyewe wana uwezo wa kifedha?

Katika mahusiano wanaume wanapaswa kutambua ishara kama hizi mapema ambazo zitakutahadharisha kuingia katika uhusiano na dada ambaye katika siku zijazo hatakuthamini;ambaye kila kizuri kitakuwa chake.Bila shaka wanaume wengi watakubaliana nami kuwa sio rahisi kubaini tabia hizi miongoni mwa akina dada,kabla ya uhusiano kunoga.Halikadahlika iwapo katika siku za kwanza za uhusiano utagundua kuwa dada ana mazoea ya kununa kwa sababu umeshindwa kutekeleza jambo fulani na kutupa matusi makali bila kuogopa,funganya virago kwani hii ni ishara atakukosea heshima siku za usoni.
Wanaume wengi hawaelewi kuwa uhusiano wa kudumu ni uwili ,kila mmoja akijitahidi kumfurahisha mwenzake .Wanajitwika jukumu la kuleta raha katika uhusiano kwa jua kwa mvua.Wamejitwika madeni ya ufukara pasi kukidhi kiu cha mwenziwe kikuacho kila uchao.Mwaunaume aingiapo matatani hutupiliwa mbali kwa madharau..Haya yananikumbusha bwana mmoja aliyeoa na kuishi na mkewe mjini .Alimtumikia kwa kila njia alipokuwa mwenye mshahara mnono.Alipofutwa kazi na mali kufifia kwa mahitaji yasiyoisha ya mkewe,mkewe alimwaibisha kwa kumfuata kila mwanaume aliyekuwa nacho na hatimaye kumtoroka kwa madai mwanamke ni kama gari.

Wanaume watakubaliana nami kuwa ni wengi wanaoishi maisha ya kunyanyaswa na wake wao bila kulalamika. Kimefika kiwango cha kupigwa,kuuawa,kutusiwa na kutishwa kupitia makundi haramu.Wengine wameendewa kwa wachawi kulainishwa wakaishia kupoteza akili zao razini.

Licha ya kishidikizo wanaume kunyenyekea na kufuatia haki za wanawake wanastahili.


Maswali
a. Eleza kilichomkera mwandishi na kwa nini? Al 2

b. Kutokana na taarifa hii ni ishara gani zinaashiria kuwa tabia kama hizi zimekita mizizi miongoni mwa wanawake. Al 3

c. Eleza sababu mbili zinazofaa kumfanya mwanaume kuvunja uhusiano mapema kulingana na mwandishi. Al 2

d. Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumika katika taarifa hii. Al 3
i. Kwa jua kwa mvua

ii. Mwanamke ni kama gari

iii. Akili zao razini

e. Wanaume wanakumbana na changamoto gani katika ndoa? Al 3

f. Andika neno lingine lenye maana sawa na yafuatayo kulingana na taarifa. Al 2
Kunoga

Pasi

C. MATUMIZI YA LUGHA
1. Bainisha maneno katika sentensi zifutazo
i. Mama anapika ugali al 3

ii. Alifika kabla ya wote

2. Bainisha viambishi vya neno lifuatalo. Al 2
Ilinyesha

3. Sahihisha sentensi hizi al 2
i. Nilimpea mkebe hizi jana.

ii. Hizi ni zikombe za kukunywa chai.

4. Unda vitenzi kutokana na nomino hizi. Al 2
i. Mtukufu

ii. Mchumba

5. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendwa al 2
i. Mzee alimwadhibu mwana kwa sababu ya utundu.

ii. Huyu paka ndiye aliyeyanywa maziwa yote.

6. Kanusha sentensi zifuatazo al 2
i. Vidozo alikula wali jana akashiba.

ii. Wavulana walicheka juzi.

7. Eleza maana ya vitate hivi. Al 4
i. Tua

ii. Dua

8. Yakinisha al 2
Wasingalisoma kwa bidii wasingalipita mtihani huo.

9. Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi hizi. Al 3
i. Yeye mwenyewe ni mwanafunzi.

ii. Ambao ulipotea umepatikana.

iii. Wangapi watafika?

10. Fafanua sauti hizi./p/ na /b/ al 2

11. Eleza maana ya: al 2
a. Kiimbo

b. Shadda

12. Andika sentensi ifuatayo kulingana na maagizo
Kuku alitaga yai.(hali timilifu) al 2

13. Onyesha aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo
Leon alikuwa akicheza uwanjani. Al 2

14. Maneno yafutayo yamo katika ngeli gani? Al 2
i. Ugwe

ii. Limau

15. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. Al 2
W+V+T+E

16. Andika katika kinyume:
Msichana mzuri alifunga mlango. Al 1

D. ISIMU JAMII (ala 10)
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
Mhudumu: Mnakaribishwa.Menyu hii hapa.Mtakula nini?
Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali.Fanya haraka
Mhudumu: Sawa mzee,Nafurahi kukuhudumia.
Mteja 2: Mhudumu,hebu leta mboga na madodo na chemsha mbili.Pia uletee maji ya machungwa.
Mhudumu: Sawa.Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza.
Mteja 1: (Akila).Wewe!please bring me drinking water.Yawe baridi tafadhali.
Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani.Glasi nayo hii pia ,karibu.
Mteja 2: Nina haraka mzee.Wapi toothpick?
Mhudumu: Hizo hapo mezani na maji.
Mteja 1: (Akila) Mhudumu ,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
Mhudumu: Naam.
Mteja 2: (Akisimama)Nimeshiba.Hizi pesa.Nilitee change haraka niondoke.

Maswali
1. Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya? Al 2

2. Taja sifa zozote nane za sajili hii. Al 8

E. FASIHI SIMULIZI
i. Andika sifa nne za visasili. Al 4

ii. (a) Hadithi ni nini? Al 2

(b)Kwa nini hadithi zilitambwa wakati wa jioni? Al 4

iii. Andika tofauti tano kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi. Al 10

 

More Examination Papers