Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Form 1 Kiswahili End of Term 2 Exams 2021

Class: Form 1

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 1 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1629     Downloads: 35

Exam Summary


JINA………………………..……………………………..NAMBARI ………DARASA…………

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI 2021
KIDATO CHA KWANZA
MUDA: SAA 2

1. UFAHAMU(Alama 15)

Ajira ya watoto
Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.Fauka ya hayo,walininginia katika umaskini uliokithiri.Hivyo,wengi waliselea katika kazi za kijungu jiko.Watot wa umri wa kwenda shule walikosa elimu na kuzurura mitaani.Udhaifu huu ulimpa faida Mwakisu,tajiri mmoja aliyemiliki shamba kubwa.Aliwaajiri watoto hao.
Mwakisu alikuwa mkwasi alietononoka si haba.Kama ni senti ,alikuwa nazo.Kilichotia doa jina lake ni kiburi.Mbali na kiburi hicho,yeye hakujaliwa moyo wa huruma na utu.
Hakubarikiwa kuwa mwema .Maadili hutuongoza kila mara kuwa ‘wema hauozi’.
Kwa Mwakisu,wema ulioza na kuvunda .Utu uling’oka katika bawaba za moyo wake na ukawa msamiati aliouchukia.Aliwatumikisha watoto wa wenzake huku wake wakisoma shule.Tabia yake hiyo ndiyo iliyowafanya Wavuruni kumtoa katika orodhayao ya watu wema.
Mwakisu alistaajabisha!Hakutaka kununua mashine zozote za kufanya kazi shambani ingawa alikuwa nao uwezo.Alistahabu kuajiri watoto wadogo na kuwadhulumu.Mkwasi huyu alifurahia kuona vitoto vikimenyana na kazi shambani kwake tangu mawio hadi machweo na hatimaye kuwapa ujira mdogo.
Siku moja Kingi alimtaka radhi, “Bosi naomba uniongezee chochote ,kwani tuna shida nyumbani.” Mwasiku alimkodolea macho huku mdomo ukimcheza.Hapo alimchomolea mwajiriwa wake tusi kubwa kutoka kwenye hazina yake isiyopungua.Tusi ambalo lilimtaabisha Kingi kulisahau.Lilikaririwa akilini mwake kwa sonono.Tangu siku hiyo Kingi akaona kuwa kuajiriwa na Mwakisu ni kufadhiliwa u chini.
Kiburi cha mwakisu kilidhihirika kila mara .Kila alipomwona motto akilia kwa uchovu au maumivu ,ungemsikia akimfokea ,”Chapa kazi!Unalilia nani hapa?Kama humudu kazi rudi kwa mamako ukanyonye.”
Kazi nyingi zilikuwa ngumu na hazikuwastahili watoto wenye umri mdogo.Si kipupwe, si kaskazi,si vuli,si kiangazi ,si kusi:kazi ziliongezeka na kuwaumiza watoto.Kingi,kwa mfano,alitakikana akame ng’ombe kumi na abebe maziwa hadi kwenye tangi kubwa .Kisha angewakatia mg’ombe nyasi na kuwasafisha .Hatimaye angehitajika kuzoa samadi.
Msimu wa kipupwe uliwadia.Baridi ikawatafuna watoto hao waliokosa mavazi bora.Kingin aliugua.Watoto wengi wakapatwa na maradhi.Wawili wakaaga dunia.Wazazi walipoona maisha ya watoto wao yamo hatarini,wakaandamana hadi kwa Mwakisu.tajiri huyo aliwajia kwa meno ya juu,’msiniitie kibuhuti.Mimi niliwaajiri watoto,sio watoto na wazazi wao”.Wazazi wakatanabahi kuwa , ‘Pa shoka hapaingii kisu’.Waliandamana hadi kwa chifu.Chifu alipoyaona yamempita kimo,akafululiza hadi kituo cha polisi.
Mwakisu akakamatwa ,akashtakiwa na kuhukumiwa .Alipatikana na makosa ya kuwaajiri watoto wenye unri mdogo na kusababisha vifo vya wawili hao.
Serikali ikatoa amri kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni.Ikatoa pia misaada ya kuendeleza elimu;elimu ya bure kwa shule za msingi.Kingi akasoma hadi kuhitimu chuo kikuu.Akawa daktari.
Alfajiri moja mahabusu waliletwa hospitali kuu ya mkoa kwa matibabu.Kingi akampa huduma mzee aliyejawa mvi na kukoboka meno.Alipomtazama kwa makini akamkumbuka.
Mwakisu akabahatisha,”sura yako….ni kama Kingi…”Kingi akamjibu,”Mimi ndiye Kingi.”Wakakondoleana macho,huku machozi yakimtiririka Mwakisu.

Maswali
1.Toa kichwa kingine kwa habari hii. (alama 1)


2.Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni. (alama 2)



3.Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao? (alama 2)



4.Taja kazi alizofanya Kingi. (alama 3)



5. Mwasiku alishtakiwa kwa makosa gani? (alama 1)


6.Eleza maana ya semi hizi. (alama 3)
(a)Kazi ya kijungu jiko.


(b)Tononoka si haba.


(c)Kodolea macho.



7.Toa maana ya methali hizi: (alama 2)
(a)Wema hauozi.


(b)Pa shoka hapaingii kisu.


8.Toa maana ya msamiati huu kama ulivyoptumiwa katika makala: (alama 1)
(a)Fauka ya (d)Alistahabu


2.MATUMIZI YA LUGHA(alama 40)
(a)Taja na utofautishe aina mbili kuu za sauti za lugha ya Kiswahili (alama 2)
Kutaja

Tofauti

(b)Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu. (alama 5)
1.PNG


c) Eleza maana ya
i)Shadda

ii)Kiimbo (alama 2)

(iii)Weka shadda neno barabara (alama 2)

Kuonyesha maana ya shwari na baraste

Shwari ______________________ Baraste_______________

(d)Taja vipashio vinne vijenzi vya lugha ya Kiswahili. (alama 4)




(e)Tenga silabi na uainishe katika neno (alama 2)
Muhtasari

(f)Sahihisha sentensi hizi
(i)Mtoto amerara usingizi mnono.

(ii)Papu yangu ni mzee kiazi. (alama 3)

(g)Tofautisha sauti . (alama 2)
/r/ na /l/


(h)Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili. (alama 3)


(i)Kamilisha methali. (alama 2)
Mgagaa na upwa ______________




(j)Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (alama 5)
(i)Mwalimu anaandika .

(ii)Mwalimu anaandika ubaoni.

(k)Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa. (alama 4)
Mofimu _______________
Viambishi_______________
(l)Andika visawe vya viwakifishi hivi. (alama 4)
(i)Nukta-

(ii)Koma –

(iii)Mkwaju-

(iv)Mtajo-



 

More Examination Papers