Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Form 3 Opener Term 3 Examination 2019

Class: Form 3

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 3 Opener Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 749     Downloads: 16

Exam Summary


Kiswahili Form 3 Opener Term 3 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


SEHEMU YA A : USHAIRI (ALAMA 20)
Soma Shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata:

VITA VYA NDIMI
Huyo !Amshike huyo!
Hakuna bunduki wala kifami
Bomu na risasi hata hawazijui
Lakini mno wanashambuliana
Kwa ndiMi zilizonolewa kwa makali
Vipande vya matusi silaha zao
Yu imara mmoja wao
Akirusha kombora la neno zito!
Linitingishe adui wake
Na kumgusa hisia kwa pigo kuu
Pigo linalochoma moyoni kama kichomi
Kuchipuza joto la hasira na kisasi
Katika mapigano yaso na kikomo
Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!
Ni nai anayekubali suluhu?
Roho zinakataa katakata
Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala kote
Mapandikizi ya watu yakipigana
Vita shadidi visivyo ukomo
Vita vya ndimi!
Magharibi sasa
Jua linapungia mkono machweo
Nalo giza likinyemelea kwa kuburi na
Kasi
Sisikii tena sauti za misonyo
Mate ya watesi yamekakuka
Makanwa yao yamelemewa na uchovu
Sasa wameshikana mikono
Ishara ya suluhu

 

More Examination Papers