Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Form 1 Opener Term 3 Examination 2019

Class: Form 1

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 1 Opener Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1335     Downloads: 30

Exam Summary


Kiswahili Form 1 Opener Term 3 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


SEHEMU YA A : UFAHAMU (ALAMA 15 )
FADHILA ZA PUNDA
Rita na Evelyn walikuwa marafiki wa chanda na pete kwa muda mrefu. Waliishi katika mtaa wa Kibokoni jijini Mombasa. Evelyn alikuwa mwanafunzi wa masomo ya uhazili katika chuo kimoja pale mjini. Naye Rita alifanya kazi ya ukarani papo hapo mjini. Waliishi kidugu katika chumba kimoja walichopanga pale mtaani. Ingawa marafiki hawa walishirikiana kwa kila njia katika shughuli za upishi, kupiga deki, kufagia, kufua na kazi nyinginezo za nyumbani, aliyekuwa akitoa msaada mkubwa zaidi alikuwa ni Rita. Rita alikuwa na mazoea ya kutunza pesa zake vyema. Aidha alijua maana ya haba na haba hujaza kibaba. Alijua kuwa Evelyn, kama mwanafunzi, hakuwa na uwezo wa kuyakidhi baadhi ya mahitaji yake. Alijitolea sabili hata kumnunulia Evelyn nguo, viatu na vim vingine alivyohitaji. Mara nyingine ilibidi Rita kulipa kodi ya nyumba peke yake kwa vile mwenzake hangeweza kupata pesa kwa wakati. Hakuwahi hata siku moja kumkera wala kumtesa Evelyn kwa jinsi yoyote ile. Fauka ya hayo, hakuwahi kumsemesha vibaya wala kuonyesha dharau kwake. Aliamini kama wanavyosema watu kuwa dunia rangi rangile, huenda siku moja atahitaji kusaidiwa yeye pia. Siku kama hiyo atamtegemea Evelyn, mwandani wake. Evelyn alipomaliza masomo yake alikuwa na bahati ya mtende. Alipata kazi nzuri mara moja katika kampuni moja ya maffita papo hapo jijini. Lakini muda si muda, mambo ya ajabu yalianza kutokea. Baada ya kupata kazi yenye kipato kizuri, kichwa cha Evelyn kilianza kufura mfano wa kaimati. Badala ya kunisaidia mwenzake katika kazi za pale nyumbani pamoja na gharama za maisha, alifhatilia raha za jijini kwa kuamini ule msemo wa ponda raha kufa kwaja. Rita alipomwuliza alimjibu kwa ukali, “Nikusaidie nini? Sasa si kama wakati nilipokuwa mwanafunzi. Kila mtu ana pesa zake.Ala!” Rita hakumwelewa tena Evelyn.Isistoshe, alianza kumwibia Rita vitu vyake wakati alipokuwa hayupo nyubani. Mara kwa mara Rita aligundua kuwa pesa alizokuwa ameficha sehemu Fulani nyumbani zimedokolewa. Alipomwuliza, Evelyn alikujajuu, “Unafikiri mimi sina pesa? Unadhani ni wewe tu uliyeajiriwa?” Rita alizidi kushangaa, Muda wote alioishi na kumfadhili rafiki yake aliamini kuwa atamlipa mema. “Kumbe fadhila za punda ni mateke?” Alijiuliza Rita. Baada ya muda, urafiki wao ulivunjika na Evelyn akahamia mtaa wa Furaha alikoendelea na maisha yake ya starehe na ureda. Hata hivyo mambo yalianza kumwendea mrama Evelyn. Wakubwa wake kazini hawakupendezwa najinsi alivyoendesha shughuli zake pale ofisini. Mara nyingi alifika kazini akiwa amechelewa na kila wakati alitoa vijisababu mbalimbali ambavyo havikumridhisha yeyote. Aidha, alipokuwa ofisini hakufanya mengi isipokuwa kutembea kutoka ofisi hii hadi nyingine akiwasumbua watu kazini mwao. Mara kwa mara alionekana akisinzia wakati wenzake walipokuwa wakichapa kazi. Lakini lililowakera zaidi wakuu wa kampuni hiyo ya mafuta ni jambo fulani lililoanza kutendeka pale. Vitu vya watu vilianza kupoteapotea.Mara mfanyikazi huyu anapoteza saa yake, mara mwingine anapoteza pesa, mara hiki mara kile. Wakuu walipoyatupa mawazo yao nyuma wakagundua kuwa mambo haya yalianza kutendeka mara tu alipowasili Evelyn. Wakaamua kumwekea mtego. Evelyn alioshikwa kimasomaso akidokoa mkoba wa msichana mwenzake. Mkoba huo ulikuwa umeaehwa juu ya dawati kimakusudi ili kumvuta Evelyn. Evelyn alifutwa kazi papo hapo. Fauka ya hayo, alitiwa mikononi na kukabidhiwa poisi waliomtupa korokoroni. Kesho yake Evelyn alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la wizi. Alitozwa faini ya shilingi elfu tano au kifungo cha miezi sita. Hakuwa na pesa zozote za kulipia faini hii. Akawekwa rumande. Hata rafiki mmoja hakuwa naye wa kumuauni katika wakati huo wa majaribu. Kwa bahati, Rita alisikia kuhusu kadhia hiyo.Hakupoteza muda. Akashika njia moja kwa moja hadi kituo cha polisi. Mpango ukafanywa na akamlipia. Evelyn ile faini. Evelyn alipoachiliwa hum akashangaa. “Yaani nimesamehewa ama nini?”Aliuliza.“La. Hujasamehewa.Faini uliyotozwa imelipwa na msichana yule.” Evelyn akageuka na kumwona Rita. Alimtazama kwa muda bila kujua la kusema. Mwishowe alimsogea kisha wakakaribiana polepole na kukumbatiana. Machozi yakaanza kumdondoka Evelyn, nde! Nde! Nde! Akalia kilio cha uchungu na soni. Akamwomba Rita msamaha, “Nisamehe, sikujua nililokuwa nikifanya.Nilidhani kuwa baada ya kupata kazi sitahitaji tena urafiki wako. Haya yaliyonipata yamenifunza,” alisema kwa masikitiko. “Evelyn, kijengacho mtu ni uth na tabia,” alisema Rita.“Ni kweli rafiki yangu” alitamka Evelyn, Sasa nimejitia kwenye shida.Hata kazi yangu nzuri nimeipoteza.Sina mahali pa kuishi. Itabidi nirudi kijijini kwa baba na mama. Kwaheri rafiki yangu naasante kwa yote uliyofanya.”“La! Hutaondoka”. Rita alimwambia lcwa dhati, “Tutakwenda nawe nyumbani mwangu tukaishi pamoja kama zamani. Nitayagharamia mahitaji yako yote hadi utakapopata kazi”. Basi Rita na Evelyn wakaungana tena na kuishi vizuri katika nyumba ile ile mtaani Kibokoni. Kweli akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.

MASWALI:
1. Maisha ya Evelyn na Rita yalikuwaje kabla ya Evelyn kupata kazi? (alama 2)

2. Kutokana na jinsi Rita alivyomtunza Evelyn, unafikiri yeye alikuwa ni mtu wa ama gani? (alama 2)

3. Eleza baadhi ya mambo ambayo Rita alimtendea mwenzake. (alama 2)

 

More Examination Papers