Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Form 1 End of Term 3 Examination 2019

Class: Form 1

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 1 End Term 3 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1750     Downloads: 25

Exam Summary


Kiswahili Form 1 End of Term 3 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


A. UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali

Ajali haina kinga. Watu wengi wanapotajiwa neno ajali, fikira zao hukimbilia moja kwa moja hadi barabarani. Mara chachemawazo yao huenda viwandani, mashambani au kwenye viwanja vya michezo. Ni nadra sana watu kufikiraia kuwa nyumbani ndiko ajali nyingi zinztokea.

Idadi kubwa ya ajali nyumbani hutokea kimchezo tu. Watu wengi wameteleza msalani na wanapata majeraha mabaya. Wengine wameteleza walipokanyaga vitu vyenye unyevu sakafuni, kama vile mafuta, mabaki ya chakula au hata maganda ya ndizi. Ulemavu walio nao watoto na hata watu wazima hutokana na ajali kama hizi wasizofikiria wtu wengi.

Ajali vilevile hutokea watu wanapozama katika shughuli au kupata jazba kuu ya kutenda. Katika hali hii, huweza kujiumiza au kuwaumiza wengine bila kujua.
Hapa tunazungumzia watu ambao hujaribu kubebe mizigo yenye uzani wasiokadiria. Madhara huwa kuteguka viungo na kuchanika misuli. Aghalabu hulemewa na kubanwa. Mwandishi wa makala haya siku moja alipanda kibao kuangika picha ukutani. Ingawa alikuwa mfupi, ari ilimsukuma kuchuchumia. Matokeo ni kibao kilijisukuma nyuma. Mhusika alianguka akajigonga kidevu. Kitendo hiki kilisababisha yeye kujiuma ulimi vibaya. Kuvunjika jino na hata kuzirai. Bahati ni kuwa alikuwepo mtu aliyempa huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitalini.

Hat hivyo ajali nyingi hutokana na vifaa vya nyumbani. Zana hizi ni pamoja na visu, meko ya gesi, mashine zinazotumia umeme na kadhalika na huwa hatari sana, hasa kwa watoto. Kitu kidogo hata kama wembe huweza kusababisha madhara makubwa. Kwa hakika hakuna yeyote kati yetu, hata waliokulia katika makasri ya fahari asiye na kovu. Makovu haya ambayo tunayaficha katika mavazi yetu ni ishara ya majeraha kutokana na ajali nyumbani. Je una kovu lolote?

Unakumbuka ulivyolipata?

Ingawa ajali hizi haziepukiki, yawezekana kuzipunguza. Ni muhimu kukuza tabia na mazoea ya kuwa waangalifu nyumbani. Kwa mfano, ni hatari kuepua chungu chenye maji yanayotokota mekoni kwa mikono mitupu. Aidha ni kutowajibika kuchanganya kitu chochote chenye unyevu na mafuta moto mekoni. Watu wengi wamebambuka ngozi na nyumba kuteketea kwa namna hii. Kwa hivyo ni vizuri kupata ujuzi wa jinsi ya kutumia vifaa na kuhakikisha tunavirudisha ipasavyo.

Jambo la tatu na muhimu zaidi ni kuwepo kwa vifaa pamoja na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza. Inawezekana kuokoa maisha au kuounguza majeraha kwa kuchukua hatua za dharura.

Maswali
1. Eleza maana ya methali ‘Ajali haina kinga’ (alama 2)
2. Kwa nini mwandishi anasema ajali nyumbani hutokea kimchezo? (alama 3)
3. Ni mambo gani mengine yanayosababisha ajali nyumbani? (alama 3)
4. Onyesha vile invyowezekana kupunguza ajali nyumbani. (alama 3)
5. Eleza maana ya: (alama 4)
(i) Jazba
(ii) Makasri
(iii) Makovu
(iv) Kuepua

 

More Examination Papers